MWENYEKITI mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufuli ameonya wanachama wanaokisaliti chama hicho na kuwataka watubu mapema au wachukue hatua za kuondoka ndani ya chama hicho.
Amesema amejipanga kuhakikisha anakomesha suala la usaliti ndani ya chama hicho, kwani baadhi ya wanachama wamekuwa wakikisaliti chama hicho.
Dk Magufuli ambaye pia ni Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameyasema hayo leo wakati akitoa hotuba ya shukani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho kumchagua kwa kishindo kuwa Mwenyekiti wa chama hicho.
Amesema ndanio ya chama hicho, kuna tabia kwa baadhi ya wanachama wao kukisaliti chama hicho kwa asubuhi kuwa wana-CCM na usiku kubadilika na kuwa wanachama wa Chadema na vyama vingine vya upinzani.
"...wasaliti wa namna hii hawatakuwa na nafasi ndani ya uongozi wangu, kama wapo watubu mapema au watupishe ndani ya chama chetu hata leo hii, ni heri kuishi na mchawi kuliko msaliti, nasema watubu au watupishe, waondoke hata leo hii," amesisitiza Dk Magufuli.
D Magufuli amesema hawahitaji kuwa na wanachama wasaliti, ambao wako ndani ya chama hicho kwa maslahi yao binafsi au kumuabudu mtu kwa maslahi yao binafsi, hivyo wanahitaji kuwa na wanachama ambao watakuwa ni Wana-CCM bila kuyumba iwe ni usiku, mchana, kwenye mvua kwa kuwa ndio misingi ya waasisi wa chama hicho, Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume.
Katika hatua nyingine, Dk Maguli ameonya wanachama wanaojihusisha na vitendo vya rushwa kuwa hatakuwa tayari kuwavumilia kwa kuwa hata katiba ya chama hicho inapiga vita vitendo vya rushwa.
"...Kama ingekuwa suala la rushwa mimi nisingeoata nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Rais, kwenye uongozi wangui ukiwa
umejipanga kupata uongozi wa rushwa hautapata nafasi, nawaomba
tujiepusha na vitendo vya rushwa, kupokea zawadi kinyume na utaratibu wa
chama. Atakayefanya hivyo chini ya uongozi wangu hatutamuoni aibu,
nitahakikisha chama kinasimamia misingi ya katiba,".
Aidha, Magufuli amegusia suala la rasimali za chama hicho, ambapo ameahidi kuunda tume ya kufuatilia rasilimali hizo ili ijulikane zinatumikaje na mapato yake yanakinufaishaje chama hicho.
Jambo lingine, amesema ni kuimarisha utendaji kazi wa chama hicho na kusema suala hilo ni muhimu sana, kama alivyokuwa akisema Mwalimu Nyerere kuwa chama legelege huzaa serikali legele, hivyo atashirikiana na wanachama hao kujenga chama kitakachosimamia vizuri serikali.
Amesema wanachama wa CCM na walioko ngazi ya chini ndio mabosi wa viongozi wote wa serikali awe Rais, waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa au watu wengine mabosi wao ni wana CCM.
"Kiongozi
yoyote atakayeshindwa kujua mabosi wake ni wanaccm na viongozi walioko
chini wajiandae kuondoka...tutahakikisha tunakuwa na safu bora katika
ngazi zote kuanzia shina hadi taifa, kwa kshirikiana na nyinyi
tutaangalia muundo, kwa kuondoa vyeo visivyo na tija ndani ya chama,
kuondoa vyeo visivyo na tija hasa wakati huu," amesema.
Pamoja na hayo Rais Magufuli pia amezungumzia mambo mengi ikiwemo masuala ya kuwaacha chipukizi wasome badala ya kuwaingiza kwenye siasa pamoja na mamsuala mengine mengi.
No comments:
Post a Comment