RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed
Shein, amefuta uteuzi wa Naibu Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar
(ZRB), Hafidh Ussi Haji.
Nafasi yake imechukuliwa na Khadija
Shamte Mzee, ambae uteuzi wake umefanywa chini ya uwezo aliopewa Rais na
kifungu cha 15(1) (A) cha sheria ya Bodi ya Mapato ya mwaka 1996 kama
ilivyorekebishwa na kifungu cha 11 cha sheria namba 2 ya mwaka 2000.
Aidha Dk. Shein, amemteua Amour Hamil Bakari kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar kuchukua nafasi ya Abdi Khamis Faki ambaye anastaafu kwa mujibu wa sheria.
Uteuzi wake umeanza Agosti 1,2016 huku uteuzi wa Naibu Kamishna ukianza Julai 25, 2016.
Dk. Shein pia amemteua Umi Aley kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali,
uteuzi ambao ameufanya chini ya kifungu cha 11(a) cha sheria namba 11 ya
2008 iliyounda Shirika hilo.
Said Bakar Jecha na Septuu Mohammed
Nassor wameteuliwa kuwa Makamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa
Umma wakati Ali Saleh Mwinyikai ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya
Utangazaji Zanzibar.
Wengine walioteuliwa ni Maryam
Hamdan kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na
Utamaduni wakati Maryam Abdulla Yussuf ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa
Baraza la Mitihani Zanzibar na Prof. Ali Seif Mshimba, ameteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Zanzibar.
Uteuzi wa viongozi hao umeanza Julai 25, 2016.
No comments:
Post a Comment