Hatimaye Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unaoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa Dodoma Convection Center (DCC) umemchagua kwa kura za Kishindo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa chama hjicho.
Akitangaza matokeo hayo, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete amesema, jumla ya kura zilizopigwa ni 2398 na kati ya hizo hakuna kura iliyoharibika.
"...Kura ya hapana ni sifuri, kura zilizoharibika ni sifuri....kwa maana hiyo namtangaza Dk John Pombe Magufuli amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi," amesema Kikwete.
Wakati wa kumkabidhi kijiti cha Uenyekiti, Kikwete amemkabidhi Dk Magufuli Ilani ya chama icho, huku akisisitiza mambo manne kuwa ndiyo vitendea kazi asmi vya Mwenyekiti huyo mpya.
"Nakupa na haya ma-book manne, hii ni tathmini ya uchaguzi mkuu uliopita, tuliofanya sisi wenyewe, tumefanikiwa vipi, hatukufanikiwa vipi, tumeapata tatizo vipi na nani alikuwa tatizo.
"Sasa utaangalia namna gani utafanyia kazi, baada ya kusema maneno hayo, mimi kazi yangu imeisha, mi uenyekiti wangu umeisha, kubalini matokeo," amesema Kikwete.
No comments:
Post a Comment