Mmiliki wa Gazeti
la Dira ya Mtanzania Alex Msama akizungumza katika mkutano na waandishi
wa habari Dar es Salaam jana wakati akimuomba radhi Waziri wa Katiba na
Sheria Dk.Harrson Mwakyembe kutokana na habari iliyochapishwa kwenye
gazeti lake la toleo namba 423 na 424.
Alex Msama akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
MMILIKI wa Gazeti la Dira ya Mtanzania
Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Harrson
Mwakyembe kutokana na habari iliyochapishwa kwenye lake toleo namba 423
na 424.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati
akiomba radhi kwa Waziri Mwakyembe, Msama alisema habari hizo zilikosa
weledi na umakini kutoka kwa mhariri na mwandishi.
Alifafanua kuwa toleo namba 424 lilikuwa
na habari yenye kichwa kisemacho "Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa
hadharani wakati toleo namba 423 ilikuwa na habari inayosema Mwakyembe
atuhumiwa kutapeli bilioni 2.
"Habari hizo zimenisikitisha mimi
binafsi na kamba Dk. Mwakyembe ni kaka yangu wa karibu na nimefahamiana
naye kwa muda mrefu. Hivyo naomba aniwie radhi kutokana na usumbufu alioupata
pamoja na familia yake,"alisema Msama.
Aliongeza tayari kama kampuni imechukua
hatua za kumsimamisha kazi mhariri na mwandishi wa habari hiyo wakati
uchunguzi ukifanyika kabla ya kuchukua hatua zaidi za kinidhamu.
Msama alisema kilichomsikitisha zaidi
hata yeye mwenyewe ni taarifa hizo kumhusisha moja kwa moja Dk. Mwakyembe
badala ya kampuni yake ya Power Pool.
Alisema kama ambavyo amekuwa akimheshimu
Dk. Mwakyembe ataendelea kumheshimuna kutambua mchango wake mkubwa kwa
taifa hili huku akisisitiza kuomba radhi kwa kilichotokea.
No comments:
Post a Comment