SERIKALI mkoani
Kilimanjaro imetaka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, kuunga jitihada za
kukuza uchumi wa mkoa huo kwa kufikisha mtandao wake maeneo ya kibiashara.
Pamoja na kukuza
uchumi, lakini pia mtandao huo umetakiwa kujaribu kuweka fursa za elimu ili
wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu kupata taarifa zitakazosaidia
kukuza taaluma.
Mkuu wa Mkoa huo,
Leonidas Gama alisema hayo wakati anafungua duka la Tigo mkoani hapa, ambalo
litakuwa likihudumia wateja 250 kila siku.
Alisema mkoa huo una
fursa za kibiashara, hivyo kuna kila sababu kwa kampuni kuitumia ili
kuwaunganisha wafanyabiashara wa mjini na vijijini kuweza kuuza na kununua
bidhaa mbalimbali.
"Mfano wilaya ya
Rombo ipo mpakani na Kenya, kuna uwezekano wa wafanyabiashara kununua na
kusambaza bidhaa kama hakuna mtandao ni
vigumu biashara kufanyika na hiyo haitakuza uchumi," alisema.
Mkuu wa mkoa alisema
kuwapo kwa mitandao ya simu, kunasaidia kupunguza matukio ya uhalifu, kwani
wananchi hususan wafanyabiashara husafirisha fedha kupitia Tigo-Pesa na
mingineyo.
Awali, Meneja Ubora wa
Huduma kwa Wateja, Mwangaza Matotola alisema duka hilo litatoa huduma za
intaneti, kadi za simu, kuuza kadi za muda wa hewani na huduma za kifedha.
No comments:
Post a Comment