Wasanii wa SHIWATA wakigaiwa maeneo ya kujenga katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga.
Wasanii
wakipata maelekezo kutoka kwa mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib
kabla ya kugaiwa nyumba zao katika awamu ya mwisho Agosti 8, mwaka huu,SHIWATA yazialika klabu, taasisi za michezo kujenga stadium, kumbi za burudani kijijini kwao Mkuranga,.
Bado kuna ekari 290 bado hajizapata matumizi
.Kila mwanachama kupewa robo hekari bure
.Jella Mtagwa, Dua Said, Hamisi Kinye ni baadhi yao.
Na Mwandishi Wetu
MIAKA
15 imepita sasa kutoka wasanii na wanamichezo walipoungana na kuacha
itikadi zao kwa kuanzisha kikundi cha kufanya maonesho ya pamoja,
kusaidiana kwa hali na mali na kutafuta makazi ya pamoja ya kudumu.
SHIWATA
inayongozwa na Mwenyekiti Cassim Taalib katika kutimiza malengo hayo
kutoka ianzishwe mwaka 2004 imekuwa ikiandaa matamasha mbalimbali katika
ukumbi wa Star Light na Lamada mkoani Dar es Salaam na katika viwanja
vya wazi kama vile Bandari Tandika na vingine kutika kuonesha sanaa ya
wanachama wake.
Baada
ya SHIWATA kusailiwa Baraza la sanaa Taifa(BASATA) mwaka 2005 pia
imesajiliwa na Mamlaka ya Leseni (BRELLA) kwa shughuli za kiuchumi ikiwa
na dira ya kuwakomboa wasanii kuwa na maisha bora kupitia mtandao huu
ifikapo mwaka 2015.
Wasanii
mbalimbali wa fani za maigizo, filamu, sarakasi, soka, bongo movie,
muziki wa taarab,bongo fleva na kung Fu wamekuwa kivutio kikubwa kila
yanapoandaliwa maonesho hayo.
Kipindi
chote ambacho maonesho hayo yakifanyika SHIWATA ilikuwa ikihaha
kutafuta njia nyingine ya kuwaendeleza wasanii wake kwa kutafuta eneo la
kujenga nyumba za makazi ya wasanii ya bei nafuu na kupata shamba
ambalo litalimwa kwa pamoja.
Mwenyekiti
Taalib anasema katika jitihada za kutafuta maeneo zilianzisha msafara
wa wasanii kutafuta eneo katika vijiji vya wilaya ya Kisarawe mkoani
Pwani.
Anasema
katika jitihada hizo lilipatikana eneo la ekari 50 katika Halmashauri
ya Wilaya ya Kisarawe katika kijiji la Visegese ambalo uliingia dosari
pale Serikali ya Wilaya ya Kisarawe iliyokuwa chini ya Mkuu wa Wilaya
hiyo wakati huo, Hanifa Karamagi kuwagomea wasanii kumiliki eneo hilo
ambalo mpaka sasa fedha zilizolipwa zaidi sh. mil. 4.1 hazijarejeshwa.
Kipindi
hicho baadhi ya wasanii waliokuwa mstari wa mbele ni pamoja na marehemu
Steven Kanumba,Mwanzo Mpango "King Kikii", Suzan Lewis "Natasha",
waandishi wa habari akina Maulid Kitenge, Peter Mwenda, Spear
Patrick,Isaac Gamba na wengine wengi.
Taalib
anasema baada ya kukwama kumilikishwa eneo hilo na Serikali ya Wilaya,
jitihada za kutafuta eneo jingine ilianza na kufanikiwa kupata ekari 300
kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi katika kijiji cha Mwanzega,
Mkuranga mkoa huo huo wa Pwani.
Anasema
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga wakati huo, Henry Clemence aliwapokea kwa
mikono miwili wasanii hao na kukubali kubariki kupatiwa eneo hilo
kulikofanywa na uongozi wa Serikali ya kijiji cha Mwanzega.
"Jitihada
ziliendelea a kutafuta mashamba ambayo wasanii watalima baada ya
kuhamia kijijini na kufanikiwa kupata ekari 500 katika kijiji cha
Ngarambe"anasema Taalib.
Anasema
SHIWATA ilianza kusafisha shamba hilo kwa gharama kubwa na kugawa ekari
tano kwa kila mwanachama iliyependa kulima lakini walishindwa
kuliendeleza kutokana na sababu mbalimbali kama vile ulinzi wa mazao
kutokana na wanyama waharibu.
Mwenyekiti
Taalib anasema wanachama waliogaiwa shamba hilo ni wale wanachama hai
waliolipia ada zao na kulipa sh. 200,000 kila ekari moja na kuongezewa
nusu ekari kila mmoja.
Baada
ya kugaiwa huko awamu ya pili ya kilimo kwanza katika shamba la Ngarambe
ili kurahisisha baada ya kutumia mtambo wa kisasa (bulldozer)
lililokodishwa kutoka Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam
kwa gharama y ash. mil. 22 kusafisha ekari 200.
"Ardhi
hiyo ina rutuba kubwa na mazao yanayostawi eneo hilo ni mpunga,
mahindi, mbaazi, viazi vitamu, ndizi, kunde, korosho, mtama na matunda
kama embe, machungwa, matikiti maji na mafenesi"anasema Taalib.
SHIWATA
yenye wanachama zaidi ya 8,000 wa fani mbalimbali za sanaa za maigizo,
mpira wa miguu, mpira wa wavu, netiboli, waigizai wa filamu, muziki wa
dansi, muziki wa kizazi kipya, vijana na waandishi wa Habari wengi wao
wameitikia ujenzio wa nyumba nafuu ambako mpaka Agosti mwaka huu nyumba
120 zimekwisha gaiwa.
Mbali
ya maonesho ya sanaa, ujenzi wa nyumba za bei nafuu za sh. 631,000
zilizojengwa kwa miti kuezekwa kwa bati ni sh. 631,000, nyumba za chumba
kimoja za saruji za sh. 750,000, nyumba za chumba kimoja na sebule sh.
3.8 na nyumba za vyumba viwili na sebule sh. mil. 6.4.
Serikali
ya Wilaya ya Mkuranga ilikitambua rasmi kijiji hicho kwa kupeleka
Mwenge wa uhuru Julai 21,2014 ukiongozwa kitaifa na Rachel Kassanda na
wasanii zaidi ya 1,500 walijitokeza kupokea ugeni huo.
Mkuu
wa wilaya hiyo kipindi hicho alikuwa Mercy Sila ambaye aalitoa
ushirikiano katika sherehe za uzinduzi wa kijiji hicho kwa kuchonga
barabara ya kufika kijijini na SHIWATA iligharimia kulipa minazi, miembe
na miti ya matunda ambayo barabara ilipita.
Mwenyekiti
pia anasema katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga wasanii wa fani ya
filamu na tamthilia ilitengeneza filamu mbili ya kwanza ya kisufuria
ambayo inaeleza maisha ya kawaida ya mtanzania na ya pili ya Ua Jeusi
ambayo inaeleza ugonjwa hatari ambao bado haujajulikana ambazo zote
zimeanza kurushwa kwenye vyombo vya habari.
Filamu
ya Kisufuria imetengenezwa na wasanii maarufu kama Lumole Matovole
"Big", Ahmed Olotu "Mzee Chilo", Haji Mboto na katika filamu ya pili ya
Ua Jeusi ni Mzee Msisi na mwigizaji maarufu Kenyata.
Taalib
anasema baada ya mafanikiop hayo changamoto iliwakuumba SHIWATA na
wamiliki wa nyumba hizo kushindwa kuhamia kijijini jambo ambalo
liliwalazimu kubuni njia nyingine ya kutoa ardhi nyiongine kwa ajili ya
kulima bustani kwa wqale ambao watakuwa tayari kuhamia kijijini.
Katika
mpango huo mwanamichezo maarufu, Dua said aliyewahi kuchezea Simba na
timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars", mchezaji wa zamani wa Yanga,
Ramadhani Kampira na mwanamuzi mkongwe King Kikii kukubali kuhamia
kijijini.
Hata
hivyo wasanii 21 walijitokeza kuuungana na wanamichezo hao kuhamia
kijijini Mwanzega, Mkuranga na kupewa chakula, mbolea ya kulima bustani
ya mbogamboga na wameanzisha kilimo cha kisasa cha pamoja kijijini hapo.
Taalib
anasema changamoto zinazoikabili SHIWATA mpaka sasa ni kutokuwa na
vifaa vya kisasa vya kilimo kama vile matrekta kwa upande wa shambani,
kutokuwa na barabara nzuri za kufika kijijini,kutokuwa na umeme, maji,
kituo cha Polisi, shule na zahanati.
"Mpaka
sasa ardhi ambayo imetumika kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi ni
ekari kumi tu bado SHIWATA imebakiwa na hekari 290 ambazo zinahitaji
uwekezaji wa klabu au taasisi kujenga viwanja vikubwa vya michezo
mbalimbali kama mpira wa miguu, mpira wa wavu, riadha na michezo mingine
inayohitaji maeneo makubwa" anasema Taalib.
Anasema
SHIWATA pia inawataka wanachama wake kuchangia fedha za ujenzi wa
nyumba zao, shule hospitali na wengine wenye wanaotaka kuchangia ujenzi
watapata robo hekari yaani miguu 35 kwa 35.
Mwenyekiti
Taalib anasema bado masharti ya kujiunga ni wale wale wanachama ambao
ni wasanii, wanamichezo na wanahabari ambao wamejiunga na mtandao huo
watapewa bure ardhi ya kujenga nyumba kutokana na uwezo wake.
Anasema
mgao wa nyumba hufanyika mara mbili kwa mwaka, kila mwezi Desemba na
mwezi Juni.Katika mgawo wa mwaka huu uliofanyika Agosti 8, mwaka huu
ambapo nyumba 16 ziligaiwa na kufikisha nyumba 120 mpaka sasa.
Baadhi
ya wacheaji wa zamani waliokabidhiwa nyumba zao ni mchezaji wa zamani
wa timu ya Pan, Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania "taifa Stars, Jella
Mtagwa, mcheaji wa zamani wa Simba, Dua Said na kipa wa Yanga, Hamisi
Kinye.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Ofisa Habari wa SHIWATA, Peter Mwenda 0715/0752 222677.
No comments:
Post a Comment