BEI ya mafuta na
petroli na dizeli imezidi kuongezeka, ambapo kwa rejareja imeongezeka kwa Sh
100 kwa lita sawa na asilimia 5.34 na Sh 88 kwa lita sawa na asilimia 5.16 huku
bei ya mafuta ya taa ikiwa haijabadilika.
Kwa kulinganisha na
mwezi uliopita, bei ya jumla kwa mafuta ya petroli na dizeli pia imeongezeka
kwa Sh 99.63 kwa lita, sawa na asilimia 5.66 na Sh 87.51 kwa lita sawa na
asilimia 5.51 huku bei ya jumla ya mafuta ya taa nayo haijabadilika.
Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi,
alisema hayo wakati akitoa taarifa kuhusu bei ya kikomo za mafuta hayo kuanzia
jana na kueleza kuwa mabadiliko hayo yametokana na kupanda kwa bei ya mafuta
katika soko la dunia .
Alisema sababu nyingine
ni kuendelea kudhoofika kwa thamani ya
shilingi dhidi ya dola ya Marekani. Pia alitaja sababu nyingine kuwa ni
kutokana na kuwa hakukuwa na mafuta ya taa yaliyoingia nchini mwezi Mei, hivyo
bidhaa hiyo itaendelea kuwa kama ilivyokuwa kwa mwezi mei mwaka huu.
Alisema vituo vyote vya
mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango
yanayoonekana bayanayakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au
promosheni zitolewazo na kituo husika.
“Pale ambapo
inawezekana kuchagua,wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye
vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani kwani ni
kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei uanyoonekana vizuri kwa wateja na
adhabu itatolewa kwa kituo husika,” alisema
No comments:
Post a Comment