Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akizungumza na maofisa ugani wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya jinsi ya kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Newala ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). Kutoka kushoto ni Mtafiti, Bestina Daniel kutoka COSTECH na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Ally Lilama.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Shakira Ahmadi, akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa wilaya kufungua mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Mji wa Newala, Calistus Komba, akizungumza kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
Mtafiti Besitina Daniel kutoka COSTECH, akiwatambulisha maofisa wenzake kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
Muonekano wa Ukumbi wa Mikutano wa Halmshauri ya Wilaya ya Newala.
Maofisa ugani wakiwa katika mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
usikivu katika mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Ally Lilama, akijitambulisha katika mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya hiyo akisoma hutuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo. Wengine waliokaa nyuma ni wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akizungumza na watafiti. Kutoka kulia ni Dk.Emmarold Mneney, Benadetha Kimata, Dk.Nicholaus Nyange, Bestina Daniel na Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia katika Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Philbert Nyinondi.
Maofisa ugani wa wilaya hiyo wakijadiliana wakati wa
mafunzo hayo.
Mwezeshaji kutoka OFAB, Dk. Emmarold Mneney, akitoa mada kuhusu matumizi ya sayansi na teknolojia katika kilimo.
Ofisa Ugani wa Mji wa Newala, Lazaro Nchai, akiuliza swali kuhusu dhana potovu ya matumizi ya bioteknolojia katika kilimo.
Ofisa Ugani wa Kata ya Chikwedu-Chipamanda, Muharami Juma Salim, akiuliza swali katika mafunzo hayo kuhusu zao za mhogo.
Ofisa kutoka Costech, Rose Soloka akiwajibika katika mafunzo hayo.
Na Dotto Mwaibale,
Newala
MKUU wa Wilaya ya
Newala, Aziza Mangosongo amesema wilaya yake inahitaji teknojia ya kisasa
ya kilimo ili kupata mazao mengi yenye tija.
Katika hatua
nyingine amesema wilaya yake imejidhatiti katika kilimo kwa kuwa na chakula
cha kutosha hivyo kutokuwepo na wasiwasi wa njaa.
Mangosongo
ameyasema hayo wilayani hapa leo wakati akifungua mafunzo ya namna ya kutumia
sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo
ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia
Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB).
Alisema wilaya
yake inahitaji teknolojia ya kisasa ya kilimo ili kuongeza tija ya kilimo
hivyo aliiomba COSTECH kufanya utaratibu wa kutoa mafunzo hayo.
Mangosongo alisema
hali ya chakula katika wilaya hiyo ni nzuri na hiyo imetokana na wananchi
kujituma na kushirikiana kwa karibu na maofisa ugani.
" Nawaombeni
maofisa ugani kuzingatia mafunzo mtakayoyapata ili yaweze kuwasaidia wakulima
wetu katika vijijini na kata mnazotoka" alisema Mangosongo.
Alisema wilaya
hiyo imepata fursa kubwa ya kupata mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa, na
kuwataka elimu watakayoipata waipeleke kwa wakulima jambo litakalosaidia kuongeza
mara dufu chakula katika wilaya hiyo.
Mwezeshaji kutoka
OFAB, Dk. Emmarold Mneney aliwaambia maofisa ugani hao kuwa wameamua kutoa
mafuzo hayo kwa kuwa wanaamini kwamba changamoto zinazokabili kilimo ni
nyingi hasa magonjwa ya mazao, wadudu waharibifu pamoja na kukosekana
kwa mvua za
kutosha.
Alisema mkulima
ili aweze kuwa na kilimo chenye tija, lazima aongezee rutuba kwenye udongo wake,
atibie mimea sawa na binadamu anavyotibiwa. Alisema sayansi ipo kwa ajili
ya kumfanya mkulima apate mazao mengi na sio kuendelea kuwa maskini
kama ilivyo sasa.
“Tuko hapa
kuelezea namna teknolojia hizi ambazo zinasaidia kukabiliana na changamoto
hizo, lengo ni kutaka wakulima wetu wazalishe kwa tija nchi ijitosheleze
kwa chakula lakini pia mkulima auze mazao yake na kupata faida,” alisema
Dk. Mneney.
Mshauri wa Jukwaa
la matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo, Dk.Nicholaus Nyange alisema
kutokana na ongezeko la watu na ardhi kuwa ile ile matumizi ya sayansi na
teknolojia
yanahitajika ili kukabiliana na ukosefu wa ardhi na ukame ambao ni changamoto
kubwa kwa wakulima hasa katika kilimo cha mahindi.
"Kutokana na
mabadiliko ya tabia nchi hali ya kilimo imebadilika hivyo ni vizuri kilimo
cha mazoea kikaachwa na kufanyika kilimo cha kitafiti chenye tija ambacho kitamwezesha
mkulima kupata magunia ya mahindi 35 ya kilo 100 kwa ekari badala ya nane"
alisema.
Mtafiti wa Mazao
ya Mizizi na Jamii ya Viazi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele
mkoani Mtwara, Benadetha Kimata, ametoa wito kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo
kutoa ushauri kwa wakulima kutumia mbegu bora za mihogo zenye ukinzani.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Philbert Nyinondi aliwajulisha washiriki wa mafunzo hayo kuwa wakulima wa Tanzania hawajabahatika kulima zao lolote lililofanyiwa uhandisi jeni.
" Hadi sasa,
hakuna mkulima wa Tanzania aliyewahi au anayelima mazao ya Uhandisi jeni (GMO),
na sio kulima tu hata wale wanaofuga, hakuna mfugaji mwenye mnyama wa GMO
Tanzania." alisema Nyinondi.
Akifafanua kauli yake Philbert Nyinondi alisema watu wengi kwa kutofahamu au kwa makusudi wanawachanganya wakulima hasa wale wanaotumia mbegu za chotara na kuwaambia ndo GMO.
"Tumefikia upotoshaji wa kiwango cha juu sana kwenye jamii. Mtu akiona kitu bora au kilichoboreshwa mfano maembe makubwa, mananasi makubwa, mimea inayokuwa kwa muda mfupi na hata kuku wa kisasa huitwa GMO. Ukweli ni kwamba labda Serikali yetu iamua wakulima wa Tanzania wafaidi teknolojia hii mapema zaidi. Vinginevo, kwa kasi ya watafiti wetu, tunaweza kuwa na zao la kwanza la GMO kwa mkulima kuanzia mwaka 2022" alisema Nyinondi.
Alitanabaisha kuwa upatikanaji wa mazao GMO hata hiyo mwaka 2022 utategemea matokeo ya utafiti unaendelea nchini, tathimini zitakazofanywa na Taasisi ya serikali kama kamati ya kusimamia matumizi salama ya bioteknolojia NBC,
Taasisi
ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Mamlaka wa Uthibiti wa Chakula na Dawa Tanzania (TFDA)
na wepesi wa kampuni za mbegu zenye usajili Tanzani kuzalisha mbegu za kutosha
kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima.
No comments:
Post a Comment