Na
Dotto Mwaibale, Masasi
WANANCHI
wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamelilalamikia Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) kutokana na kuwakatia umeme mara kwa mara na kusabisha kuungu kwa vifaa vyao vya majumbani.
Wakizungumza
na waandishi wa habari wilayani hapa leo wananchi hao walisema kuwa tabia hiyo
ya kukatiwa umeme mara kwa mara imekuwa sugu na hawajui kilio chao hicho
wakipeleke wapi.
"
Hii tabia ya kukatiwa umeme kila siku tena bila ya kupewa taarifa imekuwa sugu
hapa wilayani kwetu hatuji ni nani tumuambie" alisema Muharami Hamisi
mkazi wa mjini hapa.
Hamisi
alisema wananchi wengi wamekuwa wakiunguliwa vifaa vyao vinavyotumia umeme
zikiwemo taa lakini wanakaa kimya kwa kuwa hajui wapi waende kulalamika.
Mwajabu
Liganga alisema wanaona kama Tanesco wanawafanyia makusudi kuhusu kukatika huko
kwa umeme kwa mara kwa mara kwani wanapofika viongozi wa kitaifa katika mji huo
huwa hawakati umeme unawashwa kuanzia asubuhi hadi jioni.
"Tunashangaa
wanapofika viongozi wa kitaifa hapa wilayani umeme haukatwi lakini wakiondoka
tu hali inarudi palepale" alisema Liganga.
Liganga
aliongeza kuwa umeme huo kwa siku umekuwa ukikatwa na kuwashwa kwa zaidi ya
mara kumi bila ya kuwepo kwa maelezo ya kina.
Akizunguzia
madai hayo Ofisa Usambaji wa Umeme wa Wilaya hiyo aliyetajwa kwa jina la Iddi
Kuhanga alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo akieleza kuwa sababu kubwa ni uwezo
wa uzalishaji wa umeme huo kuwa mdogo.
Alisema
kuwa umeme unaotumika wilayani hapo unatoka mkoani Mtwara hivyo hadi ufike
Masasi unakumbana na changamoto nyingi ikiwemo ya kuharibiwa kwa
miundombinu kwa kuangukiwa na miti kutokana na shughuli za kilimo au ndege
kukaa kwenye nyaya.
Kuhanga
alikanusha madai ya kuwa wanapofika viongozi wa kitaifa hali hiyo ya kukatika
umeme huo inakuwa haipo.
No comments:
Post a Comment