Chama
cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) kimetangaza mkutano wa mkuu wa 34 wa mwaka
ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Sera za Afya kwanza katika utekelezaji wa
malengo 17 ya Maendeleo endelevu 2016-2030.
Wadau
wa maendeleo hasa idara za Serikali, Sekta Binafsi, Vyuo Vikuu, Taasisi
za Utafiti na Mashirika yasio ya kiserikali na ya kimataifa na wananchi kwa
ujumla wameombwa kuwakilisha andiko litakalosomwa kwenye mkutano huo na kisha
kujadiliwa na hata kufikia maazimio ya pamoja mkutano huo kwa mwaka huu
unatarajia kufanyika mkoani Singida.
No comments:
Post a Comment