HIZI NDIYO FAIDA ZA MCHAICHAI KWA AFYA YAKO - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, January 1, 2016

HIZI NDIYO FAIDA ZA MCHAICHAI KWA AFYA YAKO

http://2.bp.blogspot.com/-g8fdAe-rQwk/VoXi7VHgv1I/AAAAAAAAIN8/me5pHyxQV1s/s1600/Lemon%2BGrass.jpg
 
Ni wengi wanaotumia na kuufahamu mchaichai kama kiungo cha cakula jikoni na wengine hutumia kama dawa ya mbu. Lakini, je unafahamu kuwa majani haya yana aida kubwa kiafya.
 
Mafuta vya mchaichai hutumika katika viwanda vinavyotengeza pafyumu na sabuni.
 
Tafiti kadhaa zinaonesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupamban ana athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. Wengine huamini kuwa mchaichai huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli.
 
Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa. Faida nyingine za mchaichai ni pamoja na:
 
KINGA DHIDI YA SARATANI
Tafiri mbalimbali zimeonesha kuwa kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti wa Chuo Kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una uwezo wa kuua seli zinazoweza kusababisha saratani.
 
MMENG'ENYO WA CHAKULA
Husaidia umeng'enyaji wa chakula. Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng'enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi.  Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini.
 
Katika matibabu, unatibu magonjwa mengi ikiwemo kushusha joto, hasa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na malaria kali.
 
KUSAFISHA FIGO
Mchaichai pia una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu mwilini, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa kwa kemikali za kiwandani na hivyo kushindwa kuziondoa baadae kusababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani.
 
Figo inapokuwa safi na imara, hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika kirahisi kwani mkojo unapozidi kuwa mchafu mtu hujikuta akivimba mwili na wakati mwingine kufikia hata hatua ya kupoteza maisha.
 
MAUMIVU WAKATI WA HEDHI
Mchaichai pia huwasaidia akinamama ambao wanaumwa na tumbo kipindi cha hedhi, ambao wengi wao huchukulia kama change.
 
"Unapokunywa mchachai, unaweza kusafisha mirija ya uzazi na hivyo kuwezesha damu kupita kwa urahisi,".
 
MAJIPU NA MCHAFUKO WA DAMU
Vilevile mchachai una kazi ya kusafisha damu, hasa kwa watu ambao wamekuwa na tabia ya kupata magonjwa ya ngozi kama mapele na kutokwa na majipu.
 
KUZUIA KUHARISHA
Mchachai pia unaelezwa kuwa ni dawa ya kuzuia kuharisha ambapo una uwezo wa kupambana na mdudu aina ya Protozoa anayesababisha ugonjwa huo.
 
MAMA WAJAWAZITO
Endapo mjamzito atatumia majani ya mmea huu kwa muda mrefu, ataweza kujiepusha kujifungua kwa njia ya upasuaji kwani husaidia katika kulegeza nonga ambazo hubana katika kipindi cha ujauzito na kufanya njia kuwa ndogo kuwezesha motto kupita.
 
WENYE VIDONDA VYA TUMBO
Hata hivyo kwa wagonjwa wanaosumbuliwa hasa na vidonda vya tumbo, mchachai husaidia kuondoa gesi ambazo huwapata mara kwa mara.
 
HUONGEZA CD4
Kwa wagonjwa wa Ukimwi, mchaichai unaelezwa kuwa unasaidia kuongeza CD4 na inashauriwa kuwa ni vyema mgonjwa wa aina hiyo akapendelea kutumia zaidi mchaichai kulio majani ya chai.
 
 
Makala hayo yameandikwa kwa hisani ya MZIZI MKAVI BLOG
 


3 comments:

Post Top Ad

Responsive Ads Here