WAZIRI WA AFYA AFANYA ZIARA BOHARI YA DAWA (MSD) - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, January 1, 2016

WAZIRI WA AFYA AFANYA ZIARA BOHARI YA DAWA (MSD)

Waziriwa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisalimiana na viongozi mbalimbli wa Bohari ya Dawa (MSD) Dar es Salaam .
 Hapa Waziri Mwalimu (wa pili kushoto), akifanya mkutano na menejimenti ya MSD. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk.Donan Mmbando na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, Profesa Idrisa Mtulia.
     Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Mwalimu wakati alikitembelea ghala la dawa la MSD.

 Na Mwandishi Wetu.

WAZIRI wa Afya ,MaendeleoyaJamii, JinsiaWazeenaWatotoMhe. Ummy Mwalimu ametembelea Makao Makuu ya Bohariya Dawa (MSD) nakuahidi kuwa balozi wa kuhakikisha deni la serika lilinalipwa ilikuiwezesha MSD kutekelezama jukumu yake kwa ufanisi.

Wazirihuyoameelezahayobaadaya Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu kueleza kuwa ukosefu wa fedha na deni la serikalinichangamotokubwainayoathiriutekelezajimzuriwamajukumuya MSD.

Mbali na hilo, waziri huyo wa Afya amesema mbali na den ihilo, hata kiasi cha fedha kinachotengwa na serikali kwa ajili ya Hospitali, vituo vya Afya na zahanati kununua dawa hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala hilo lifanyiwe kazi mapema, huku akisistiza hata kiasi hicho kidogo kinachopatika na kitumike vizuri.

Katika hatua nyingine ameishauri Bohari ya Dawa kuanza utaratibu wakununua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kuhakikisha dawa muhimu zina patikana wakati wote na kuiagiza MSD itangaze kwenye vyombo vya habari dawa zote ambazo zinapelekwa vituoni, zahanati na kwenye hospitali, ambapo Mkurugenzi Mkuuwa MSD Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa tayari MSD imeshaanza kubandika kwenye mbao za matangazo za hospitali orodha ya dawa inazofikisha.

Waziri huyo ambaye alifuatanana Katibu Mkuu wa Wizara yake na watendaji wengine alitembelea maghala ya kuhifadhia dawa yaMakao Makuu, jengo la ofisi linalojengwa pamoja na kuwa na mkutano na menejimentiya MSD, ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza MSD kwa hatua iliyofikia ya kuweka nembo ya GOT kwenye vidonge vyake ilikudhibiti upotevu wa dawa za serikali pamoja na kuanzisha maduka ya dawa Muhimbili, namengine yanayotarajia kufunguliwa hivi karibuni mkoani Mbeya, ArushanaMwanza.

Wazir iUmmy Mwalimu alihitimisha kwa kusema kuwa ajenda yake kuu niupatikanaji wa dawa kwa wakati, kama rais wa Jamhuri yaMuunganowa Tanzania Mhe. John Magufuli alivyo aainisha, hivyo MSD itekeleze majukumu yake ipasavyo kwani mafanikioya MSD nimafanikio kwake pia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here