HOSPITALI Teule ya Rufaa ya mkoa wa Pwani ya Tumbi
itanufaika na upatikanaji wa vifaa kupitia mradi wa usalama kwa wagonjwa kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu cha RKU cha nchini Ujerumani.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini
kwake mjini Kibaha, Ofisa habari wa Shirika la Elimu Kibaha ambalo ndilo
wamiliki wa hospitali hiyo, Lucy Semindu alisema kuwa mbali ya kunufaika na
vifaa pia itanufaika na wataalamu toka chuo hicho.
Semindu alisema kuwa tayari mradi huo umeanza kwa
wataalamu kutoka chuo hicho kuitembelea hospitali hiyo wiki iliyopita na
kujionea hali halisi ya utoaji huduma.
“Mkataba wa mradi huo uliingiwa mwaka jana utasaidia
upatikanaji wa vifaa tiba na kwenye utoaji huduma kuanzia kuwapokea wagonjwa,
kuwapatia dawa, upatikanaji wa vifaa vya taka pamoja na kubadilishana uzoefu
ambapo wataalamu wa Tanzania nao watatembelea Hospitali ya chuo hicho,”
alisema.
Aidha alisema kuwa hospitali hiyo ya Chuo Kikuu RKU
ni maarufu kwa kutibu wagonjwa wenye kiharusi na magonjwa mengine, ni tegemeo
kubwa kwa Ujerumani na asilimia 100 ya wagonjwa wanaotibiwa ni wa bima na
wanapatiwa chakula bure.
No comments:
Post a Comment