WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema utalii wa picha na
uwindaji unaofanyika katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba nchini
yanaliingizia taifa zaidi ya Sh bilioni 50 kila mwaka, huku akibainisha kuwa
utalii utaongezeka maradufu mwaka huu.
Aidha,
utalii uliingiza asilimia 18 ya pato lote la taifa huku asilimia 25 ya fedha za
kigeni zilitokana na utalii uliofanyika katika kipindi cha mwaka uliopita.
Profesa
Maghembe amebainisha hayo wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji
cha Kizi kilichopo katika Wilaya ya Nkasi akiwa katika siku yake ya pili katika
ziara yake ya kikazi mkoani Rukwa.
Akiwa
njiani kwenda katika Kijiji cha Kizi alisimama kwa muda katika Kijiji cha
Lyazumbi na kuzungumza na wananchi, vijiji hivyo viwili vinapakana na Pori la
Akiba la Lwafi ambalo lina vitalu vya uwindaji wa kitalii.
“Mwaka
huu kumekucha utalii unatarajiwa kuongezeka maradufu, muhimu wananchi kwa
kushirikiana na askari wa wanyamapori endeleni kulilinda pori hili la akiba ni
muhimu sana. Acheni kuvamia na kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo uchomaji
mkaa, ufugaji na ujenzi wa makazi, kunasababisha uharibifu mkubwa,” amesisitiza.
No comments:
Post a Comment