JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umepongeza mafanikio ya shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi na kuanza kwa shughuli ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi, bomba hilo
lenye urefu wa kilometa 1,445 ambalo litakuwa na uwezo wa kusafirisha mapipa
216,000 kwa siku likiwa na thamani ya Sh tilirioni nane, ni fursa kubwa
kibiashara hususani kwa wanawake.
“Mradi
huu unakadiriwa kutoa fursa za ajira zaidi ya 30,000 kwa wananchi pamoja na kutoa
fursa mbalimbali za kibiashara haswa kwa wanawake hii ni hatua kubwa sana kwa
nchi yetu hasa kwetu wanawake,” amesema
Makilagi.
Amesema mradi huo ni hatua nyingine ya kimaendeleo yenye kuimarisha uhusiano wa kindugu
na kibiashara baina ya nchi za Afrika Mashariki inayofanikishwa na Rais John
Magufuli kwa kushirikiana na Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Aidha,
UWT imempongeza Magufuli kwa hatua ya kuwapatanisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba na
kusema kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa ujenzi wa taifa la amani lenye watu
wenye upendo na walioshikamana.
No comments:
Post a Comment