SERIKALI wilayani Mbarali mkoani Mbeya imeagiza vijiji vyote wilayani hapa kuanza ujenzi wa zahanati kuanzia mwezi huu ili kuendana na agizo la serikali la kila kijiji kuwa na zahanati na kituo cha afya kwa kata.
Mkuu wa
Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune ametoa agizo hilo kwenye kikao cha Baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo.
Mfune
amesema agizo la kila kijiji kuwa na zahanati ni la muda mrefu na ni jambo la
kushangaza kuna baadhi ya vijiji havijaanza kutekeleza agizo hilo mpaka sasa.
Amesema
jengo la zahanati ni sawa na nyumba ya mtu mmoja hivyo ni jambo lisilowezekana
kwa kijiji kizima kushindwa kujenga nyumba hiyo.
“Kuanzia
mwezi huu kila kijiji kianze ujenzi kama tutashindwa baadaye huko mbele sawa,
lakini tuwe tumeonesha nia ya kujenga. Haiwezekani nyumba ya mtu mmoja kijiji
kizima kishindwe kujenga.
“Nina
imani tuna kianzio kizuri kwani kila kijiji kina benki ya tofauti. Tutumie hizo
hizo zilizopo kuanza ujenzi. Lakini pia kwa vijiji ambavyo tayari vina zahanati
ni wakati wa kuanza mradi mwingine wowote wakati wenzao wakihangaikia zahanati,” amesema.
No comments:
Post a Comment