;;
Watoto wa Chuo waliowahi kuishi chuoni hapo wakiwa kwenye picha ya pamoja hakika hii ilikuwa ni party ya nguvu.
Watoto wa chuo waliokuwa wakiishi katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wazazi wao wakiwa ni
wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ili kuweka ukaribu watoto
hao wamekutana na kufanya party ya nguvu hivi karibuni katika viwanja
vya UDSM hii ikiwa ni kurudisha ukaribu pamoja na kufahamiana kwa wale
waliopotezana miaka kadhaa chuoni hapo.
Hakika ilikuwa ni siku ya furaha maana watu walikuwa wanakumbushana mambo ya miaka ya 90 kwani kipindi hicho walikuwa wadogo.
Watoto wakiendelea kucheza wakati wa
party ya watoto walioishi chuoni hapo kipindi wazazi wao bado ni waalimu
katika chuo cha UDSM
Watoto wa wahadhiri wa UDSM
wakibadilishana mawazo kwenye party ya kuwaunganisha pamoja kama
wanafamilia wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Hakika watoto walikuwa waki-enjoy vya
kutosha maana hakuna aliyeboreka kwani kulikuwa na kila aina ya michezo
kwa watoto wa rika zote.
Baadhi ya watoto wakiwa wametokelezea kwenye ukodak.
Baadhi ya watoto walioishi Chuoni UDSM
wakiangalia vitabu pamoja na kununua vitabu hii ikiwa ni kundeleza
utamaduni wa kujisomea.
Hakika ilikuwa shangwe kwa watoto walioishi chuoni hapo wakati wazazi wao ni wahadhiri chuoni hapo
Hivi ni Baadhi ya vitabu vilivyokuwa vinauzwa wakati wa Party hiyo iliyofanyika chuoni hapo.
Muda wa kuserebuka ulifika sasa kila mtu akaanza kuonesha umahiri wake kwenye kulisakata Rhumba.
Watoto wa Chuo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza party yao.
No comments:
Post a Comment