Na Haji Nassor, Pemba
WATU
360 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na ajali 4,291 za barabarani,
zilizotokea Unguja na Pemba, kuanzia kipindi cha mwaka 2008 hadi mwezi
disemba mwaka 2014.
Kwa
mujibu wa ripoti za haki za binadamu za miaka saba iliopita,
zinaonyesha kuwa, katika kipindi hicho watu wengine 3,195 walijeruhiwa
baada ya kutokezea ajali hizo.
Ripoti
hizio zinazotayarishwa kila mwaka na Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), kwa kushirikiana na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar
(ZLSC), zinaonyesha kuwa kila mwaka, matukio ya vifo vya ajali
barabarani yanaongezeka.
Ripoti
ya mwaka 2008 imeonyesha kuwa, jumla ya watu 48 walipoteza maisha na
409 walijeruhiwa baada ya kutokezea ajli za barabarani, ambapo mwaka
uliofuata (2009), iliongezeka watu sita (6) na kufikia 54, ingawa mwaka
2010, kulipungua watu wawili wawili sawa na mwaka 2011 ambapo kulikuwa
na watu 50 waliofariki.
Aidha
taarifa za ripoti hizo za haki za binadamu, zinaonyesha mwaka mwengine
uliowaacha wazanzibari na simanzi kubwa ni 2011, baada ya kuripotiwa
idadi hiyo, na 440 kujeruhiwa, ingawa miaka miwili iliofuta kulipungua
na kuwepo watu 39 na 29 kwa mwaka 2013, huku mwaka 2014 ikipanda mara
dufu na kufikia 88, sawa na majeruhi 547.
Zanzibar
ambayo kwa mujibu wa sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2012, inaidadi
ya watu 1,303,569 ambapo kutokana na watu 360 waliopoteza maisha pekee
kwa sababu za barabarani kwa kipindi cha miaka saba iliopita, ni sawa na
kwamba mwaka mmoja kulikua na jali moja kila siku.
Aidha
kutokana na idadi hiyo ya vifo, nazo ajali 4,291 za barabarani
ziliripotiwa kwenye ripoti hizo, kuanzia kipindi cha miaka saba
iliopita, na mwaka jana ndio kulikoripotiwa ajali nyingi, kwa kufikia
845, huku mwaka 2010 zikifikia 692.
Mwaka
mwengine ulioripotiwa ajali nyingi za barabarani ni 2011 kwa kuripotiwa
615, ukifuatiwa na mwaka 2009 ajali 583, wakati mwaka 2008
zikijumuishwa ajali 536, ikikaribiana na mwaka 2013 kulikoripitiwa ajali
534 na majeruhi 503 wa Unguja na Pemba.
Kwa
mujibu wa ripoti hizo, chanzo cha kujitokeza kwa ajali hizo ni kuwepo
kwa mchanganyiko wa matumizi ya barabara, baina watembea kwa miguu,
waendesha vyombo vya magurudumu mawili na gari za kawaida.
Sababu
nyengine ni ubovu na uchakavu wa barabara katika maeneo kadhaa ya
Zanzibar, uwembamba wa barabara zenyewe, sheria za usalama barabarani
kutochukua nafasi yake na kukosekana kwa usalama mzuri sambamba na
uendeshaji wa uzembe.
Dereva
wa gari Chake chake-Mkoani Juma Mohamed ‘J’ alisema yeye anaona sababu
kubwa na ufinyu wa barabara ambao hauhimili tena ongezeko la vyombo vya
moto kisiwani Pemba.
Nae
Ali Mjaka Hashim, alisema inawezekana pia harufu ya rushwa iliopo kwa
baadhi ya wasimamizi wa sheria barabarani ndio zinazotoa fursa kwa
madereva kuendesha mwendo kasi ambapo hata akisababisha ajali hana
hakika ya kuadhibiwa.
“Madereva
hawafungwi na wala hawana adhabu kali wanapofanya makosa ya barabarani
hata kama wamesababisha kifo, ndio maana ongezeko la ajali na vifo
lipo’’,alifafanua.
Hata
hivyo baadhi ya wananchi wameshauri kuendelea kutolewa kwa elimu ya
usalama barabarani kwa waendesha vyombo vya moto na watembea kwa miguu
ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima.
No comments:
Post a Comment