Na Magreth
Kinabo- MAELEZO.
Serikali
imeanzisha utaratibu wa utoaji wa taarifa ya ugonjwa wa kipindipindu kwa wiki kwa nchi nzima
ili kuweza kuhabarisha umma wa Watanzania kwamba ni mkoa upi au wilaya
ipi imejitahidi kukabiliana na ugonjwa huo.
Utaratibu umeanza rasmi leo, tarehe 28. 12.
2015, hivyo kila Jumatatu ya wiki kama leo taarifa za ugonjwa huo zitakuwa
zinatolewa.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya ugonjwa
huo nchini kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
‘’Ninatoa
rai kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha kwamba wanaleta taarifa sahihi za watu waliathirika na mlipuko
wa ugonjwa wa kipindupindu kwani kuficha
taarifa haitasaidia kwa kuwa ugonjwa huu unaendelea kusambaa katika maeneo
mbalimbali ya nchi yetu,’’ alisema Waziri huyo.
Aidha Serikali
imesema kwamba wizara
hiyo kwa itashirikiana na wadau mbalimbali, ambao ni Ofisi ya Waziri
Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Wizara ya Maji na
Umwagiliaji, Wizara ya Elimu ya Sayansi, Teknolojia na Ufundi, DAWASCO, DAWASA
na Sekretarieti ya Mkoa wa Draes Salaam, wakiwemo wadau wa
maendeleo ili kuweza kukabiliana na
ugonjwa huo.
Akizungumzia
kuhusu ugonjwa huo, Waziri Ummy alisema
tangu umeanza Agosti 15, mwaka 2015 jijini Dares Salaam,ambapo mpaka
Desemba 27, mwaka huu umesambaa katika mikoa 21 ya Tanzania Bara.
‘’ Watu walioathiriwa na ugonjwa huo tangu umeibuka
ni 12,222 na jumla ya watu 196 wamefariki kutokana na ugonjwa huo, lakini mikoa ya Mtwara, Njombe na Ruvuma
mpaka hakuna ripoti ya watu waliathiriwa na ugonjwa huo,’’ alisisitiza.
Hata hivyo
waziri huyo aliongeza kwamba katika
kipindi cha mwezi nzima mikoa ya Kilimanjaro na Iringa hakuna taarifa za
ugonjwa huo, hivyo aliipongeza kwa juhudi walizofanya za kuudhibiti.
Waziri huyo alifafanua kwamba kwa kipindi cha
wiki kuanzia Desemba 21 hadi Desemba 27 mwaka huu jumla wagonjwa 493
wameripotiwa kuugua ugonjwa huo na vifo sita katika wilaya 46 zilizopo kwenye
mikoa 18.
Aliongeza kwamba mikoa inayoonesha kuwa na idadi
kubwa ya wagonjwa ni Morogoro(98), Mara (83),
Arusha(60)Singida(48) ,Mwanza (45) na Manyara 27 na mikoa ambayo katika kipindi
cha wiki hiyo ambayo haijaathirika na ugonjwa huo ni Iringa, Shinyanga,
Kilimanajaro, Pwani na Kagera.
Aliwataka wananchi kutumia kanuni za afya za
kunawa mikono kablaya ya kula, kunywa maji safi
na salama, kuepuka kula vyakula vilivyoandaliwa pasipo kuzingatia mazingira safi na salama , kuchaemsha maji ya
kunywa kuwa vyoo bora ili kuweza kukabiliana na ugonjwa huo.
Akizungumzia
kuhusu suala la uzoaji wa taka kufuatia zoezi la kampeni ya usafi wa mazingira
lililofanyika hivi karibuni kwa agizo la
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli, alisema watashirikiana na TAMISEMI ilikuhakikisha taka hizo
zinazolewa. Hata hivyo alisema tayari Waziri husika ameshato siku 21
kukabiliana na tatizo hilo
No comments:
Post a Comment