TANZIA: MWANDISHI MKONGWE WA HABARI ZA MICHEZO AFARIKI DUNIA - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, December 4, 2015

TANZIA: MWANDISHI MKONGWE WA HABARI ZA MICHEZO AFARIKI DUNIA

Marehemu Willie ‘Willy’ Chiwango (aliyesimama) enzi za uhai wake
Marehemu Willie ‘Willy’ Chiwango (aliyesimama) enzi za uhai wake




Habari wadau, nasikitika kuwajulisha kuwa tumepata msiba wa mwanafamilia mwenzetu na mwanataaluma wa siku nyingi katika uandishi wa habari za michezo nchini, Willie ‘Willy’ Chiwango.



Chiwango alifariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Massana, Dar es Salaam na msiba upo nyumbani kwake Ilala Mchikichini, Dar es Salaam, ambapo mipango ya maziko inafanyika.



Wakati wa uhai wake marehemu Chiwango alifanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti ya serikali, Daily News na Sunday News. Pia amepata kufanya kazi This Day na vyombo vingine.



Kwa wanaohitaji taarifa za msiba huu, namba za wahusika ni mtoto wa marehemu 0659-353006, kama ukimkosa hata mjane wa marehemu pia anazungumza kwa namba ya simu 0652-722173.



Naomba tushirikiane na familia katika kipindi hiki kigumu. Mungu amuweke mahali pema peponi marehemu Mzee Willy Chiwango, Amina.



Ahsanteni,

Katibu Mkuu TASWA.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here