Ziko simu za kisasa ambazo teknolojia
yake inaruhusu kukutana na maji na haiharibiki lakini sio simu zote
zina uwezo huo !! Nakukutanisha na headlines za Wajapan ambao wameamua
kuja na simu ambayo utaweza kuisafisha kwa maji na sabuni.
Japan wamethibitisha kwamba simu hizo zimepewa jina la Digno Rafre na zitazinduliwa rasmi wiki ijayo na kuingia kwenye rekodi za kuwa simu ya kwanza yenye uwezo wa kusafishwa kwa maji.
Hii ni nukuu ya alichokisema Boss wa Kampuni hiyo >>> “Timu yetu ilijaribu kuziosha simu hizo zaidi ya mara 700 kwa ajili ya kupima uimara wake.”
Hii hapa video ya tangazo la simu yenyewe mtu wangu.
No comments:
Post a Comment