Kamishna
wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi, Hosea Mbise akizungumza
katika mkutano wa tatu wa wawekezaji na wadau wa nishati ya umeme
ujulikanao kwa jina la Powering Africa uliodhaminiwa na kampuni ya Wind
East Africa.
Mkurugenzi
na Mwanzilishi wa kampuni ya Six Telecoms Rashid Shamte akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na mradi wa umeme wa upepo wa Singida
kupitia kampuni ya Wind EA ambao unatarajiwa kuanza uzalishaji rasmi
mwishoni mwa mwaka 2017. Shamte alisema hayo wakati wa mkutano wa tatu
wa kimataifa wa kuiwezesha Afrika katika utatuzi wa nishati ya umeme
umefanyika Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Mradi huo, Mark
Gammons.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Wind East Africa John Chaggama
akifafanua jambo kuhusiana na uwekezaji wao wa Umeme wa Upepo uliopo
mkoani Singida. Chaggama alisema mradi huo utatatua tatizo la nishati
hiyo hapa nchini mara utakapoanza rasmi uzalishaji mwishoni mwa mwaka
2017.
Wadau
na wawekezaji mbali mbali wa nishati ya umeme wakimsikiliza Kamishna wa
Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi, Hosea Mbise hayupo pichani
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tatu wa wawekezaji na wadau wa nishati
ya umeme ujulikanao kwa jina la Powering Africa uliodhaminiwa na
kampuni ya Wind East Africa.
……………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Wakati
Serikali ikibainisha kuliondoa Shirika la umeme nchini (Tanesco) katika
uzalishaji wa umeme, kampuni ya kuzalisha umeme wa upepo (Wind East
Africa) imesema itaanza uzalishaji wa nishati hiyo mwishoni mwa mwaka
ujao.
Wakizungumza
katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya umeme,
Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi, Hosea Mbise na
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa wa kampuni ya Wind East Africa, Rashid
Shamte walieleza mkakati uliopo katika kuboresha sekta ya umeme nchini
ambapo baada ya muda, Tanesco itakuwa na kazi ya usafirishaji tu huku
kazi ya uzalishaji ikifanywa na kampuni kama Wind EA.
Mbise
alisema kuwa alisema uzalishaji wa umeme unahitaji uwekezaji wa hali ya
juu ikiwamo kutoa fursa kwa kampuni mbalimbali kuanza kuzalisha umeme
kwa manufaa ya Taifa.
Kwa
mujibu wa Mbise, hatua za awali za kuliondoa Shirika hilo la umeme
nchini kuwa mzalishaji wa nishati hiyo umeanza na ifikapo 2022, Shirika
hilo halitajihusisha na uzalishaji wa umeme zaidi ya kazi ya
usafirishaji tu.
“Kwa
utaratibu huu, Tanesco sasa itaondoshwa katika mchakato wa kuzalisha
umeme na kubaki kuwa msambazaji, hatua tayari zimeanza kwa kuangalia
madeni yaliyopo Tanesco na jinsi ya kuyafuta sanjari na kuwachukua
watumishi wa Tanesco.
“Ifikapo
2022 hatutakuwa na Tanesco katika uzalishaji wa umeme bali umeme
utazalishwa na kampuni mbalimbali na mkakati uliopo ni kwamba hadi
kufikia 2030, asilimia 70 ya Watanzania wawe wamefikiwa na huduma ya
umeme,” alisema Mbise.
Kwa
upande wake, Shamte alieleza kuwa mradi wa umeme wa upepo wa Singida
kwa sasa upo katika maandalizi ya kina kuanza na mwaka ujao
watakamilisha taratibu mbalimbali kwa mujibu wa sheria za uwekezaji.
Shamte
alisema kuwa mradi huo ambao utazalisha 100 Mega Watts mbali ya kutatua
tatizo la umeme, utaufanya mkoa wa Singida kubadilika kwa kupata
maendeleo makubwa kiuchumi, biashara na hata kijamii.
Alisema kuwa mkataba mikataba ya kumalizia uwekezaji wamradi huo itasainiwa mwanzoni mwa mwezi ujao (Januari 2017).
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Wind East Africa, John Chagama
alisema, mradi wa umeme wa upepo utakapokamilika utawanufaisha
Watanzania hasa wakazi wa Singida ambako mradi huo unaanzishwa.
“Kwanza
utasaidia kutoa ajira kwa wakazi wa Singida, lakini pia utawanufaisha
Watanzania hasa wa kipato cha chini kwani umeme utakuwa wa gharama
nafuu,” alisema.
Chagama
alisema kuwa umeme wa upepo ni mradi wa kudumu na utawafanya watanzania
kupunguza gharama za maisha kwani bei ya umeme itashuka
No comments:
Post a Comment