Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wadau wa Sekta Binafsi na kuwaahidi kuwapa ushirikiano mkubwa kwani anatambua mchango wao katika ukuaji wa uchumi na kuwasihi kuwa wazalendo katika suala la utoaji kodi ili kulipeleka taifa katika nchi yenye uchumi wa Kati Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Hassan Silayo Maelezo)
………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………….
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amewapa siku
saba kuanzia tarehe 03/12/2015 wafanyabiashara wote ambao waliingiza
mizigo yao bila kulipa kodi wakalipe kwani baada ya hapo watachukuliwa
hatua kali za kisheria.
Hayo
yamesemwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam na Mheshimiwa Rais katika
mkutano wake na wadau wa sekta binafsi alipoamua kufanya mazungumzo nao
pamoja na kuwasikiliza maoni yao ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika
kipindi cha kampeni za kuomba kura za kiti cha Urais,lengo likiwa ni
kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta binafsi.
Mheshimiwa
Rais aliendelea kusema kuwa katika kipindi hichi cha miaka mitano
amedhamiria kuijenga nchi na watu wasimuelewe vibaya kwa maamuzi
anayofanya kwani ni kwania njema ya kuleta maendeleo na siyo ujeuri.
“Tutaangalia
namna ya kupunguza utitiri wa ushuru katika bidhaa mbalimbali,mfano
katika kipindi cha kampeni niligundua katika Mkoa wa Kagera na
Kilimanjaro wanakolima zao la Kahawa,wamekuwa wakitozwa tozo 26 kwa zao
hilo na hiyo imechangia kusababisha wafanyabiashara wa zao hilo kufanya
biashara haramu ya kupeleka zao hilo kwa magendo kuuza katika nchi
jirani”,alisema Mheshiwa Rais Dkt. Magufuli.
Pamoja
na hayo Mheshimiwa Dkt.Magufuli amewaahidi wadau wasekta binafsi
ushirikiano mkubwa kwani anatambua mchango wao katika kukuza uchumi na
pia amewataka wadau hao kuwa wazalendo na kuliacha kukwepa kulipa kodi
ili tuweze kujenga taifa lenye maendeleo makubwa ya kiuchumi.
Mheshimiwa
Rais Dkt.Magufuli ameendelea kusema kuwa kama kutakuwa na mfayabiashara
yeyote atakayetaka kuwekeza na akakwamishwa na mtu aliyechini ya uteuzi
wake basi mtu huyo ataondoka kwani sasa ni wakati wa wadau wa sekta
binafsi kuanza kuanzisha viwanda mbalimbali vitakavyo toa ajira.
Pamoja
na hayo Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli amewapa mawazo ya kibiashara
wadau wa sekta binafsi kuanzisha kampuni ya kutenganisha udongo unaotoka
kwenye machimbo ya madini,kuanzisha viwanda vya samaki pembezoni mwa
bahari pamoja na kutengeneza samani zitokanazo na mazao ya misitu.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw.Regnald
Mengi amesema kuwa wako tayari kumpa ushirikiano mkubwa Mheshimiwa Rais
katika kuhakikisha uchumi watanzania unakuwa kwa haraka na pia amemuomba
mheshimiwa rais kuendelea kukemea masuala ya rushwa pamoja kusaidia
kupunguza utitiri wa kodi
No comments:
Post a Comment