Na Dk. Geoffrey C. Lusanzu
Kwa walio wengi, ulaji wa nyama ni jambo lisiloshtua mioyo kutokana na mazoea ya ulaji wa chakula hiki. Wengi wetu chakula cha nyama ni kitamu sana na inaweza kushangaza mno endapo utaandaa sherehe isiyokuwa na mlo wa nyama, lakini kiutaalam nyama sio chakula rafiki wa mwili wa mtu kwa kuwa ina tindikali. Mwili ni alikalaini, kwa maana hii nyama ni mpinzani wa mwili.
Licha ya kutokuwepo upatanifu huu, nyama za wanyama na samaki zina kiwango kikubwa cha lehemu ambayo ni mafuta mabaya (cholesterol). Mafuta haya yanapouzinga mwili, huharibu damu, misuli ya damu na viungo vya mwili na husababisha maradhi makali na kifo. Jamii ya wanyama inaugua mno na hata wanapochinjwa nyama zao hukokota vimelea vya maradhi lukuki.
Kwa kawaida, nyama inapoliwa huingia tumboni na huoza huku ikitengeneza usaha unaonuka (putrid mass), kisha hufyonzwa na kuingia katika mkondo wa damu na kuidhoofisha damu. Daima ni tabia ya nyama kuidhoofisha damu kwa kiwango kikubwa.
Tafiti mbalimbali zimethibitisha vema kwamba ulaji wa nyama za aina zote (wanyama, samaki na ndege) ni hatari kwa afya ya binadamu kwa sababu nyama zimesheheni vimelea wengi wa maradhi. Ni wanyama kama ndege na samaki wachache ambao hawajaambukizwa maradhi. Kutokana na tafiti hizi binadamu anaweza kuendelea kula nyama za wanyama kwa hasara ya nafsi yake kwani vimelea wa maradhi hawana utani au urafiki na mtu yeyote.
Hii ni kwa sababu huweza kuharibu afya ya mtu yeyote pasipo kujali rika, elimu, madaraka, utajiri au umasikini. Je, ni maradhi gani yanayopatikana kwa ulaji wa nyama? Haijalishi unakula nyama kwa kiwango kipi; kidogo au sana kabisa. Hata ulaji wa nyama wa kawaida unaweza kukusababishia ugojwa mkali na kupelekea ulemavu au kifo cha mapema.
Nyama ina wadudu wabaya kama vile bakteria, ‘salmonella’, ‘listeria’, ‘campylobacter’, ‘clostridium’, ‘perfringens’ na ‘yersinia. Vimela hawa huweza kusababisha maradhi ya minyoo ndoano (hookworms), ‘rabies’, kipindupindu, tegu ya samaki, tegu ya nguruwe, kuhara damu, maradhi makali ya figo, baridi yabisi na maradhi ya ini.
Maradhi mengine yanayotokana na ulaji wa nyama ni gauti, vijiwe katika kibofu nyongo na figo, kichwa kuuma na kisichosikia dawa, saratani ya damu (leukemia). Pia husababisha saratani nyingine zaidi ya kumi (melanoma na ‘lymphoma’), ukichaa (mad cow disease). Saratani ya tezi dume (prostate cancer), saratani ya tumbo, mfumo wa kinga ya mwili dhaifu, kirusi cha hunta, maradhi ya Hodgkin, maradhi ya ‘paget’, ‘leptospirosis’, homa kali pamoja na kuvimba (bubonic plague), ‘anthrax’, ‘trichinosis’, minyoo mviringo (round worms), ‘brucelosis’, kifua kikuu, ukoma.
Magonjwa mengine ni kifafa, homa kali, matutuo, akili butu, tegu wa ng’ombe, minyoo midogo iliyobapa (ring worms), hali ya unyama na uzezeta, homa kali pamoja na uvimbe (tularemia), kuharisha maji na kuumia tumbo (cryptosporidiosis). Maradhi yote haya humwinda binadamu mlaji wa kitoweo cha nyama.
Wakati umefika sasa wa kutafakari, kupunguza ulaji wa nyama au kuanza kusaka elimu ya afya ili kujikita katika matumizi ya chakula mbadala wa nyama na kukiacha kabisa chakula cha nyama. Daima tumia chakula bora cha asili ili kujikinga na maradhi haya yaliyo hatari mno na yanaleta vifo vya mapema mno.
KWA MAKALA MBALIMBALI KUHUSU AFYA BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment