Vijana Shilen Dawda (kushoto) na Alyanz Nasser wakiwaonesha mifuko hiyo wanahabari wakati wakiitambulisha rasmi Dar es Salaam leo mchana.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Mkurugenzi wa Masoko LTD, Constantine Magavila (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habri katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Julius Ningu, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana katika utambulisho wa mifuko mbadala wa mifuko ya plastiki inayotunza mazingira ambayo imebuniwa na vijana wawili, Shilen Dawda (kushoto) na Alyanz Nasser (katikati), ambao ni wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Vijana Shilen Dawda (kushoto) na Alyanz Nasser (katikati), wakimkabidhi , Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Julius Ningu, mifuko mbadala wa mifuko ya plastiki “Rambo), inayotunza mazingira ambayo wameibuni baada ya kuitambulisha rasmi kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana.
Kijana Shilen Dawda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wakitambulisha mifuko mbadala wa mifuko ya plastiki inayotunza mazingira ambayo wameibuni na mwenzake Alyanz Nasser (kulia), ambao ni wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imewamwagia sifa vijana wawili wakazi wa Dar es
Salaam kwa ugunduzi wao unaoenda sambamba na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano
chini ya Rais John Magufuli ya utunzaji wa mazingira.
Vijana hao ndugu wenye umri wa miaka 14; Alyanz Nasser na Shilen
Dawda, wameingiza katika soko la Tanzania aina ya mifuko mbadala ya plastiki
ikiwa ni baada ya kufahamu kuwa Tanzania, hususan Dar es Salaam, lipo tatizo
kubwa la kimazingira linalohitaji ufumbuzi wa haraka.
Envirobags ni mifuko inayoweza kutumika hata zaidi ya mara
tatu tofauti na mifuko ya plastiki iliyopo sasa kwani kinachoshauriwa kwa
watumiaji ni kukumbuka kwenda na mifuko hii ya kisasa iwe supermarket au sokoni
kufanya manunuzi.
Akizungumza katika hafla fupi ya kuitambulisha mifuko hiyo
iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Msaidizi (Idara ya Udhibiti
wa Uchafuzi wa Mazingira) wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Julius Ningu, alisema:
“Vijana hawa wameonyesha mfano unaopaswa kuigwa na wadau wote
wa mazingira na sisi kama serikali, tunaahidi kushirikiana nao kuhakikisha
mazingira yetu yanabaki masafi na salama daima.”
Dk. Ningu aliwataka wadau wengine kujitokeza na kuanzisha
miradi ya aina hiyo kwa lengo la kutunza mazingira kwa kuhakikisha Watanzania hawatumii
mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku (less 30 microns) na wala haizalishwi.
Alisema mwaka 2013, serikali ilitunga sheria inayopiga
marufuku uzalishaji, usambazaji, uingizaji na zaidi matumizi ya mifuko ya
plastiki inayochafua mazingira. Zaidi ya mifuko milioni moja hutumika nchini
kila mwaka.
“Ile inayoweza kutumika zaidi ya mara moja ni asilimia ndogo
sana na mara nyingi mifuko hiyo hutupwa na kuishia kwenye maeneo kama fukwe za
bahari, ambako hudumu kwa zaidi ya miaka 1,000 ikiharibu mfumo wa mazingira,”
alisema Dk. Ningu.
Wakizungumza na waandishi wa habari waliokuwapo wakati wa
tukio, vijana waliogundua mifuko hiyo, Alyanz na Shilen, walisema walitiwa moyo
sana na uamuzi wa rais Magufuli alioufanya mapema mwezi huu wa kuwaongoza
wananchi kusafisha jiji.
“Kutokana na kupigwa
marufuku mifuko ya plastiki na juhudi za hivi karibuni za rais kuokoa mazingira,
tukaona kwamba ipo haja ya kuwa na mifuko mbadala rafiki wa mazingira. Ni hapo
ndipo tukaja na EnviroBags,” alisema Alyanz.
Alisema mifuko hiyo wataiuza kwenye supermarket kubwa nchini
wakitarajia kuwa itapunguza matumiza ya kila siku ya mifuko ya plastiki.
“Tunatumaini matumizi ya mifuko hii mipya itakuwa na matokeo
chanya kwa taifa letu na hivyo kuweza kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs),”
alisema Shilen kwa niaba ya mwenzake.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
No comments:
Post a Comment