POP UP BONGO KUFANYIKA JUMAMOSI HII TRINITI OYSTERBAY DAR ES SALAAM - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, November 24, 2015

POP UP BONGO KUFANYIKA JUMAMOSI HII TRINITI OYSTERBAY DAR ES SALAAM

Nuya Essence
Founder of Branoz Collection Bahati Abraham with customers
Secret Habits Seller servings customers
Pediah John, Founder of PSJ Brand with customers copy
  *****************
Na Mwandishi Wetu
WASANII mbalimbali wa muziki na maigizo pamoja na wadau wengine wa biashara watajumuika pamoja Triniti, Oyster bay katika  tamasha la biashara za bidhaa mbalimbali, Pop Up Bongo. 

Tamasha hilo linalofanyika kila baada ya miezi mitatu ni la siku moja na mwaka huu litafanyika tarehe 28 likiwa chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff.  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Akizungumzia kuhusiana na tamasha hilo mmoja kati ya waanzilishi wake, Natasha Stambuli alisema kuwa milango itafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi na kuwa linatarajiwa kumalizika saa mbili usiku.

Alisema kuwa ikiwa ni kuelekea msimu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya tamasha hilo linawakutanisha watu mbalimbali na wamiliki wa maduka na wafanyabiashara za aina mbalimbali. 

Alikuwa inakuwa ni nafasi nzuri kwa watu mbalimbali pia kukutana na mbali na kufanyika kwa biashara kwenye eneo hilo lakini pia inakuwa ni fursa ya kuburudika kwa kuwa kutakuwa na muziki na vinwaji hivyo kuongeza furaha kwa watakaojitokeza. 

"Ni mwishoni mwa mwaka tunaelekea na kama mnavyojua kunakuwa na mambo mbalimbali wakati tukielekea kufunga mwaka vijana wanataka kujua wapi pa kununua bidhaa mbalimbali kama nguo na vinginevyo na Pop Up bongo inawapatia fursa hiyo hapo Novemba 27" alisema Natasha.

Aliongeza kuwa "kwa mwaka huu wasanii pia wapo ambao watafika kuonana nao wadau wengine wa bidhaa zinazowahusu kama nguo na nyinginezo na hakuna kiingilio kabisa.

Alisema kuwa wafanyabiashara ambao kwa mwaka huu wataonesha bidhaa zao ni pamoja na Secret Habits, KAYA African Collection, Nuya’s Essence, HIGHSUPDSM, FT boutique, Branoz Collections, ATSU, Dress Kitenge, American Nails na wengineo wengi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here