Mgeni rasmi, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya
Afya na Usitawi wa Jamii akiwahutubia Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa
Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakati wa hafla
fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani
Kilimanjaro.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akielezea umuhimu wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na
Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya
utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi
wa Sensa na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu
akitoa maelezo ya awali wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika
leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Baadhi
ya Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na
Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati
wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani
Kilimanjaro.
Mgeni
rasmi, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya Afya na
Usitawi wa Jamii (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasimamizi,
Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania
wa mwaka 2015 mara baada ya kufunga mafunzo ya utafiti huo wilayani Moshi, Kilimanjaro.
(PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).
Wito umetolewa kwa viongozi wote wa
Serikali katika Ngazi zote na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa
Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na
Malaria utakaoanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015.
Wito
huo uletolewa leo na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Dkt. Ahmed Makuwani wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti
huo iliyofanyika wilayani Moshi, Kilimanjaro.
"Ninawaomba Wananchi kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa Wadadisi, Wasimamizi na Wahariri watakaoshiriki zoezi la kukusanya
Takwimu za Utafiti wa Afya ya Uzazi na
Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ili kupata taarifa muhimu na sahihi kwa
ajili ya kupanga Mipango na Sera endelevu za Sekta ya Afya katika nchi yetu,
amesema Makuwani".
Dkt. Makuwani amesema kuwa taarifa
zitakazokusanywa kwa wananchi kwa ajili ya
utafiti huo zitakuwa ni siri na zitatumika kwa shughuli za Kitakwimu tu
na wala hazina uhusiano wowote na Uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema utafiti huu wa Afya ya
Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015
unalenga kukusanya taarifa nyingi za sekta ya afya zinazotumika katika
kutathmini malengo mbalimbali na pia kusaidia katika kupanga mikakati mipya.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mara
nyingine tena inafanya Utafiti wa Afya
ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ambao kwa mara ya mwisho
ulifanyika mwaka 2010. Utafiti huu utaanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015 kwa
nchi nzima na utamalizika mwishoni mwa Mwezi Februari 2016.
No comments:
Post a Comment