WAZIRI
wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, (anayeshughulikia masuala ya Muungano), Samia
sSuluhu Hassan,(wapili kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania,
TPB, Sabasaba Moshingi, (wakwanza kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Property
International Ltd, (PIL), Abdulkarim Haleem, (watatu kulia), na Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Uwekezaji, Gabriel Silayo, (wane kulia), wakiwa wamekamata mwamvuli ikiwa ni
ishara ya umoja, kwenye uzinduzi wa mpango wa kukopesha viwanja wanachama wa
PSPF ambapo TPB itaratibu ukopeshwaji huo kwa kutoa fedha. Uzinduzi huo
ulifanyika jijini Dar es Salaam Jumanne Agosti 18, 2015.
Mgeni rasmi, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano), Samia Suluhu Hassan, akitoa hotuba
Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo,
Gabriel Silayo, akitoa hotuba yake
Afisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya Posta, TPB, Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba yake
Msanii wa muziki wa
majigambo, Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa PSPF, akitoa burudani kwenye
hafla hiyo.
Mh. Samia Suluhu Hassa,
akimpongeza Silayo baada ya kutoa hotuba yake. Wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji
Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi,(kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa PIL,
Abdulkarim Haleem.
NA K-VIS MEDIA
MFUKO
wa wa Pensheni wa PSPF kwa
kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania, TPB, na Taasisi ya Property
International Ltd leo Agosti 18, 2015 wamezindua mpango maalum wa kutoa
mikopo
ya viwanja kwa wanachama wa mfuko huo katika hafla iliyofanyika Hoteli
ya Hyatt Regency.
Lengo la mkopo huu wa viwanja ili kuwawezesha
wanachama wa mfuko huu kumiliki viwanja vilivyopimwa na vilivyo halali kwa
mujibu wa taratibu za nchi. Nia ni kwenda sambamba na dira ya PSPF ambayo ni
kutoa huduma bora zenye ushindani katika sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wateja wa PSPF, na pia kuitikia
mwito wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),walioagiza
Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kutoa mafao kwa fomula iliyo sawa kwa watumishi
wote. Hivyo kuanzia wakati huo Mifuko ya Hifadhi inapaswa kushindana kwa ubora
wa huduma na vivutio vingine kwa wananchama na wananchama watarajiwa.
Ni dhahiri kuwa kila Mtanzania anahitaji kuwa na
makazi bora ya kudumu, hivyo mpango huu unaozinduliwa leo hii ni mpango mzuri
sana hasa kwa Watanzania wengi ambao hawana uwezo wa kutoa fedha taslimu.
Utaratibuu huu wa kuwakopesha utawanufaisha wengi na hatimaye kufikia kauli mbiu ya Serekali
yetu ya kuhakikisha Maisha bora kwa kila Mtanzania.
Mfuko wa Penshini wa PSPF umeendeleza ushirikiano wake
mzuri na Benki ya Posta Tanzania, ambapo kama mnavyofahamu ushirikiano wao
ulianzia kwenye utoaji wa Mikopo kwa Wastaafu, Mkopo wa Elimu na Mkopo wa
kuanzia Maisha kwa wanachama wapya. Jitihada hizi zote ni katika kuhakikisha
inatoa huduma bora kwa wanachama wake, na pia katika kuonesha imani kwa Benki
ya Posta, ambayo huduma zake bora zinapatikana kote nchini. Mahusiano haya na
Property International Ltd yanazidi kujenga mahusiano haya kwa maslahi ya
wanachama na Watanzania kwa ujumla.
Wanachama wa PSPF waliochangia Mfuko kwa kipindi
kisichopungua miezi sita wanasifa zote za kuweza kukopa viwanja hivi, na
watapaswa kulipa ndani ya miaka mitatu. Wanachama walio katika mpango wa
Uchangiaji wa Hiari pia watafaidika na mkopo huu. Wanachama wote wa Mfuko wa
Hifadhi wa PSPF wanakaribishwa sana kupata mkopo huu maalum kwa ajili yao.
Mgeni Rasmi, akiwa
katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSPF
Mgeni rasmi, Samia,
akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TPB
- Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PIL
Moshingi, (kushoto), akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa PIL Zohra Moore, (kulia
Mh. Samia, (kulia), akisindikizwa na Silayo, wakati akiondoka ukumbi wa Hotel ya Hyatt, baada ya hafla hiyo
Moshingi (kulia), akisalimiana na Mh. Samia Suluhu Hassan, wakati akiwasili kwenye hafla hiyo
No comments:
Post a Comment