Wachezaji
wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es Salaam,
wakiwa katika mazoezi ya pamoja yanayoendelea kwenye Uwanja wa Karume
jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki kati
yao na timu ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa Arusha unaotarajiwa kuchezwa
mwishoni mwa mwezi huu.
Mbali
na mchezo huo pia timu hizo zinatarajia kufanya shughuli za Kijamii,
ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa na Vituo vya Albino kwa lengo la
kudumisha Amani na Mshikamano Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka
huu unaotarajia kufanyika Oktoba 25.
Mazoezi yakiendelea
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akishiriki
katika mazoezi ya pamoja na timu yake yaliyofanyika leo asubuhi kwenye
Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Kontroo imelala hapa…….
Mbona wa Arusha watakoma…..
Mazoezi ya viungo……
Kuweka misuli sawa…..
Mazoezi ya viungo….
Baadhi ya Wachezaji wakizungumza na kocha wao baada ya mazoezi…..
Mazoezi ya viungo……..
Picha Na www.sufianimafoto.com
No comments:
Post a Comment