Mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria
kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom nchini (VPL) utachezwa
kesho jumamosi katika uwanja wa Taifasaa 10 kamili jioni, ambapo
utazikutanisha timu za Azam FC dhidi ya Yanga zote kutoka jijini Dar es
salaam.
Tiketi za mchezo huo zitaanza
kuuzwa kesho asubuhi katika magari maalum maeneo ya uwanja wa Taifa,
ambapo kiingilio cha chini kitakua shilingi elfu saba (7,000) na
kiingilio cha juu ni shilingi elfu thelathini (30000) kwa VIP A.
Kuelekea mchezo huo maandalizi
yote yamekamilika, ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha, wapenzi na
wadau wa mpira wanaombwa kujitokeza kushuhudia mchezo huo. Vimininika,
silaha au vitu vinavyoweza kuhatarisha usalama havitaruhusiwa kuingia
uwanjani.
Kabla ya mchezo kati ya Azam FC
dhidi ya Yanga SC kutakua na mchezo wa utangulizi utakaozikutanisha timu
ya wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa (Taifa Stars Legends) dhidi ya
Ukonga Veterani.
Milango ya uwanja wa Taifa itakua
wazi kuanzia majira ya saa 5 kamilia asubuhi kutoka nafasi kwa wapenzi
wa mpira kuweza kuingia uwanjani mapema.
No comments:
Post a Comment