Mfamasia
Mkuu wa Serikali Dkt. Habib Ali Sharif akitoa nasaha zake kwa Maafisa wa Afya (hawapo
pichani) juu ya kuzitunza vyema Pikipiki tano zilizotolewa Msaada na Shirika linaloshugulikia
Idadi ya Watu Dunia UNFPA kwa Wizara ya Afya.
Waziri wa Afya Zanzibar Rashid Seif Suleiman akikabidhiwa funguo
pikipiki na Afisa Dhamana wa UNFPA Zanzibar Dkt. Azzah katika hafla ya
makabidhiano yaliyofanyika Bohari kuu ya Madawa Maruhubi Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Rashid Seif Suleiman akiijaribu moja ya
pikipiki zilizotelewa msaada na Shirika linaloshugulikia Idadi ya Watu
Dunia (UNFPA). Picha na Abdalla Omar-Maelezo.
Waziri wa
Afya Zanzibar Rashid Seif Suleiman akitia saini hati ya Makabidhiano ya
Pikipiki tano zilizotolewa Msaada na Shirika linaloshugulikia Idadi ya Watu
Dunia UNFPA,(kulia) Afisa Dhamana UNFPA Zanzibar Dkt. Azzah Nofly, kushoto
ya Waziri ni Mfamasia Mkuu wa Serikali Dkt. Habib Ali Sharif na Mkurugenzi wa
Bohari Kuu ya Dawa Zahor Ali Hamad. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar.
Na Faki
Mjaka-Maelezo Zanzibar-
Shirika linaloshugulikia
Idadi ya Watu Dunia UNFPA limekabidhi Wizara ya Afya Zanzibar Pikipiki tano
zenye thamani ya Shilingi Milion 12 kwa ajili ya kusaidia huduma za Afya ya
Uzazi, kwa akina Mama, Vijana na Watoto.
Akizungumza katika
Makabidhiano ya Pikipiki hizo Afisa Dhamana UNFPA Zanzibar Dkt. Azzah Nofly amesema
Msaada huo ni mwendelezo wa Shirika hilo wa kuisaidia Sekta ya Afya kuimarisha
afya za Wananchi wa Zanzibar.
Amesema Pikipiki
hizo zitatumika pia kusaidia usambazaji na usimamizi wa Dawa nchini ambapo
Maafisa wa Afya watazitumia ipasavyo katika kutekeleza majukumu hayo.
Amefahamisha
kuwa baadhi ya Vifo vya akina Mama na Watoto vinaweza kuepukwa iwapo patakuwa
na upatikanaji wa Dawa muhimu za kuokolea maisha katika Vituo husika.
Amesema Shirika
la UNFPA hamu yake nikuona kila Mimba inayobebwa inakuwa salama kwa Wazazi na Watoto
wanaozaliwa wanakuwa na Afya njema zinazopelekea kutimiza matarajio yao.
Kwa upande
wake Waziri wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif amesema uwepo wa usafiri wa uhakika
ndio unaopelekea usimamizi na usambazaji wa Madawa jambo linalopelekea kuimarika
kwa Sekta ya Afya Nchini.
Ametoa wito kwa
Mashirika mengine duniani kuiga mfano wa UNFPA katika kuisaidia Sekta hiyo
muhimu.Awali Mfamasia
Mkuu wa Serikali Dkt. Habib Ali Sharif amefahamisha kuwa Sekta ya Afya Zanzibar
inaendelea kuimarika kila siku licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali
ikiwemo ya usafiri.
“Sekta ya
Afya inaendelea vyema na tunashukuru sana kwa kuwa na Dawa za kutosha tatizo
letu ni utaratibu usiokidhi haja wa Usambazaji na usimamizi wa Dawa hizo”
Alisema Mfamasia Habib.
Hata hivyo
amedai kuwa upatikanaji wa Pikipiki hizo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza
Tatizo la Uhaba wa Dawa vituoni kwani Maafisa wa Afya watafanya kazi zao kwa
ufanisi.
Shirika la
UNFPA limekuwa likifanya kazi zake kwa karibu na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
hasa katika Wizara ya Afya ambapo September
mwaka jana pia lilitoa Magari manne ya kubebea Wagonjwa kwa Wizara hiyo.
No comments:
Post a Comment