Mhe.
Jaji Ferdinand Wambali (aliyesimama), Mkuu wa Chuo cha
Mahakama Lushoto (IJA),akitoa mada juu ya utendaji kazi katika Mahakama
katika mafunzo yaliyoanza kufanyika mapema leo katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Shaban Ali Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (katikati)
akitoa neno la utangulizi katika Semina ya Mafunzo elekezi kwa Wahe.
Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania walioapishwa hivi karibuni,
aliyeketi kushoto ni Mhe. Anold Nsekela, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya
Rufani (T) kulia ni Mhe. Salvatory Bongole, Kaimu Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Mhe.
Shaban Ali Lila, Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (katikati)
Mhe. Anold Nsekela, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe.
Salvatory Bongole, Kaimu Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji wapya wa Mahakama
Kuu ya Tanzania walioapishwa hivi karibuni, Majaji hao wapo katika
mafunzo elekezi yenye lengo la kuwawezesha sheria mbalimbali na taratibu
za Kimahakama. Mafunzo haya yataendelea kufanyika katika Chuo cha
Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) kuanzia tarehe 24.08.2015 ambapo mada
mbalimbali zitatolewa ili kuwawezesha Wahe. Majaji hao kuifahamu
Mahakama, ikiwa ni pamoja na misingi na taratibu za utoaji huduma ya
haki nchini. (Picha na Mahakama).
No comments:
Post a Comment