PICHA
iliyopigwa kutoka angani leo Jumapili Agosti 16, 2015, ikionyesha umati
mkubwa wa wananchi waliofurika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza kwenye
mkutano wa hadhara wa kumtambulisha mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, akipeperusha bendera ya
muungano wa vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA, Mh. Edward
Lowassa, na mgombea mwenza wake, Juma Duni Haji. Mh. Lowassa yuko katika
ziara ya kutafuta wadhamini baada ya kuchukua fomu Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, NEC, akiiomba imteue kuwa mgombea wa nafasi hiyo kwenye
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu wa 2015. (Picha
na Othman Michuzi wa Mtaa Kwa Mtaa Blog)
Mh. Lowassa, akihutubia mkutano huo
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe, akihutubia mkutano huo
Mh. Lowassa, na mgombea mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji
MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KUSIMAMIA HAKI YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, WCF, Masha Mshomba, akizungumza kwenye mkutano na waandishi
wa habari makao makuu ya Mfuko huo barabara ya Bagamoyyo jijini Dar es
Salaam, Agosti 16, 2015. Mfuko huo ulioanzishwa kwa sheria ya bunge
namba 20 kifungu cha 5 ya mwaka 2008, una madhumuni ya kutoa fidia kwa
Wafanyakazi kutokana na ulemavu au vifo viinavyosababishwa na ajali au
magonjwa yatokanayo na kazi sambamba na kukuza mbinu za kuzuia matukio
ya ajali, alisema. (Picha na K-VIS MEDIA)
Mfuko huo ambao umeanza kazi rasmi Julai 1, 2015, lengo kuu ni kutekeleza nia ya Serikali kukabiliana na changamoto za ulipaji wa fidia kwa Wafanyakazi katika mfumo wa utoaji fidia uliokuwepo awali, Mkurugenzi Mkuu Masha alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kiwango kidogo cha malipo ya fidia(kiwango kisichozidi shilingi 180,000) kwa ulemavu wa kudumu na shilingi 83,000 kwa wategemezi endapo kifo kitatokea kwa Mfanyakazi husika. Akinukuu sheria iliyoanzasha Mfuko huo, Masha alisema, kifungu cha pili (2), cha sheria ya fidia kwa wafanyakazi namba 20/2008 Mfuko huu unawahusu Waajiri na Wafanyakazi wote katika sekta ya Umma na Binafsi, Tanzania Bara pekee. "Naomba ieleweke, anayepaswa kuchangia kwa mujibu wa sheria hii ni Mwajiri na sio Mfanyakazi kukatwa mshahara wake." Alifafanua Masha
Mfuko huo ambao umeanza kazi rasmi Julai 1, 2015, lengo kuu ni kutekeleza nia ya Serikali kukabiliana na changamoto za ulipaji wa fidia kwa Wafanyakazi katika mfumo wa utoaji fidia uliokuwepo awali, Mkurugenzi Mkuu Masha alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kiwango kidogo cha malipo ya fidia(kiwango kisichozidi shilingi 180,000) kwa ulemavu wa kudumu na shilingi 83,000 kwa wategemezi endapo kifo kitatokea kwa Mfanyakazi husika. Akinukuu sheria iliyoanzasha Mfuko huo, Masha alisema, kifungu cha pili (2), cha sheria ya fidia kwa wafanyakazi namba 20/2008 Mfuko huu unawahusu Waajiri na Wafanyakazi wote katika sekta ya Umma na Binafsi, Tanzania Bara pekee. "Naomba ieleweke, anayepaswa kuchangia kwa mujibu wa sheria hii ni Mwajiri na sio Mfanyakazi kukatwa mshahara wake." Alifafanua Masha
Waandishi wa Habari kazini
Mwandishi kazini
Masha (katikati), akiwa na Kaimu
Mkurugenzi wa hifadhi za Jamii kutoka Wizara ya Kazi na Ajira, Daudi
Kaali, (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya
Kusimamia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini, SSRA, Ansgar Mushi
Mwandishi kazini
Waandishi wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha
Mkurugenzi Mkuu, akitoa ufafanuzi kufuatia maswali ya waandishi wa habari
You might also like:
MTAKATIFU TOM AWATEMA DAMAYO, MSUVA, NSAJIGWA KIKOSI CHA ...
Waziri wa maendeleo ya biashara Netherlands azindua vifaa ...
MSAADA ZAIDI WATOLEWA NA TBL MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA ...
TBL YAANZISHA PROGRAMU YA MAFUNZO YA KUENDELEZA WAUZAJI ...
KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM NAPE NNAUYE AZUNGUMZA ...
WAZAZI MATINEJA WAHITIMU ELIMU MBADALA
Second Secretary wa Ubalozi wa
Japan, Noriko TANAKA (kulia) akipokea kitabu cha wageni kutoka kwa
Mratibu wa kata ya Segese iliyopo halmashauri ya Msalala, wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga, Bi. Victoria Maige alipofikia katika ofisi hizo
kwa ajili ya zoezi la kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea
kwenye mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule
kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na
UNESCO.
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WAZAZI wenye umri mdogo 149 mkoani
Shinyanga ambao walipata mimba wakiwa shuleni wamekamilisha mafunzo ya
miaka miwili ya stadi mbalimbali za maisha mkoani hapa.
Wazazi hao wenye umri mdogo ni
miongoni mwa wazazi 220 walioanza mafunzo hayo miaka miwili iliyopita
chini ya mradi wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu
za Ujauzito unaofadhiliwa na Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Wazazi hao vijana kutoka wilaya tatu
za mkoa wa Shinyanga za halmashauri ya Shinyanga, Msalala na Kahama
walikuwa wanajifunza katika vituo 10.
Wengine walishindwa kuhitimisha mafunzo yao kwa sababu tofauti.
Pamoja na kumaliza mafunzo hayo na
wengine kujiandaa kwa masomo ya sekondari, wanafunzi hao walijifunza
shughuli mbalimbali ambazo zinawawezesha kujiajiri na kuongeza kipato
kwa familia zao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Msalala, Vivian Masangya alisema pamoja na akimama wadogo hao wengine
walishindwa kukamilisha masomo yao kutokana na utoro uliosababishwa na
familia, umbali wa vituo husika na wawezeshaji kuwa na posho ndogo ya
kuwezesha mafunzo kumekuwepo na mafanikio makubwa.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu
ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (kulia) akisaini kitabu cha wageni
katika ofisi za kata ya Segese iliyopo halmashauri ya Msalala, wilayani
Kahama mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo. Kushoto kwake ni
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis
Mafuniko na kushoto ni Mratibu wa kata ya Segese iliyopo halmashauri ya
Msalala, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Bi. Victoria Maige.
Alisema pamoja na changamoto hizo
mradi huo umesaidia kurejesha heshima na uwezo wa akina mama hao wadogo
na kuonesha njia kwa wengine ambao wamejikuta katika mazingira kama ya
hao waliohitimu.
Alisema mila potofu za kuozesha
mabinti wadogo na kuwabebea majukumu ya uzazi wakiwa wadogo na kisha
wengine kukimbiwa na wale waliowapa ujauzito amefurahishwa sana kuona
kwamba waliobaki wamehitimu kwa kishindo.
Naye Ofisa mipango ya Elimu wa
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta
, akimwakilisha Mkuu wa Ofisi ya UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues
alisema amefurahishwa na kukamilika kwa mradi huo ambao ulipokea dola
400,000 kutoka kwa serikali ya Japan.
Alisema mradi huo umetokana na
mahitaji ya Tanzania katika kukabiliana na tatizo la elimu kwa wasichana
wanaokatishwa ndoto zao kwa kupata ujauzito au kuolewa wakiwa wadogo.
“kama Unesco hatuna mradi. Mradi
unakuwa wa serikali wanaeleza tatizo tunakaa pamoja tunaliangalia na
kuona namna ya kulitatua” alisema Kotta wakati akisema ubunifu wa mradi
huo ambao ulikuwa na lengo la kusaidia wasichana kufikia usawa wa jinsia
kwa kuwa ukimwezesha kielimu mtoto wa kike utakuwa umeelimisha familia
na mwisho taifa.
Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika
la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta
(kulia) akimkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima
MOEVT, Salum Mjagila alipowasili kwenye ukumbi yalipofanyika mahafali ya
Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za
Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Aliwataka wahitimu kutoacha
kuyatumia mafunzo yao kwa kuwa tayari wamekuwa na msingi sasa wanaweza
kusonga mbele katika kusaka elimu.
Alisema wameshapata elimu ya kujitambua na wanachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kwamba hawabaki nyuma katika jamii yao.
“..Tumefunguliwa njia na sasa ni
lazima hatua nyingine kufikia ustawi… tukaze mwendo kwa kutumia taasisi
za elimu ili kufikia ndoto zetu za kielimu” alisema Kotta.
Naye Second Secretary wa Ubalozi wa
Japan, Dk. Noriko Tanaka akizungumza kwa niaba ya balozi wake alisema
kwamba serikali ya Japan imefurahishwa na jinsi msaada wake ulivyotumika
kuwawezesha akina wadogo kujitambua na kutengeneza mustakabali wa
maisha yao.
Alisema katika hotuba yake kwamba
anaamini wanawake hao wataanza maisha mapya baada ya kuhitimu na
kuonesha tofauti ambayo itasaidia kuwajenga wao kifamilia na kiuchumi.
Meza kuu katika mahafali ya
Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za
Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Alisema dola 400,000 zilizotolewa
kupitia Mfuko wa Pamoja wa Japan na Unesco ni sehemu tu ya juhudi za
Japan kusaidia wale waliokwamishwa katika maendeleo yao kwa sababu
mbalimbali waweze kujitambua na kushiriki katika kujiendeleza na
kuendeleza taifa.
Aidha alisema katika juhudi hizo
hizo hivi karibuni walifungua hosteli ya wasichana ambayo wanaamini
itasaidia kuondoa tatizo la wasichana wa shule kukaa na kuwakwepesha
na mimba zisizoza lazima.
Alisema ni lengo la ubalozi wake
kuhakikisha wanawawezesha wasichana kuwa na nafasi sawa kielimu katika
kuambatana na malengo ya millennia.
Mkurugenzi wa halmashauri ya
Shinyanga Vijijini Julius Mlongo, Juni mwaka huu alisema kwamba takwimu
zinaonesha kwamba Shinyanga inaoongoza kwa mimba za utotoni nchini.
Alisema hali hiyo inatokana na wazazi wengi kushindwa kuwahimiza mabinti zao kwenda shule.
Takwimu duniani zinaonesha kwamba
wanawake milioni 400 wenye umri wa miaka 20-49 au zaidi ya asilimia 40
waliolewa wakati wakiwa wadogo.
Second Secretary wa Ubalozi wa
Japan, Noriko TANAKA akizungumzia ufadhili wao wa dola 400,000 kwa ajili
ya mradi wa elimu mbadala kwa wasichana walioacha shule kwa sababu za
ujauzito wakati wa Mahafali ya Mradi huo mwishoni mwa wiki. Akina mama
wadogo 149 walihitimu elimu hiyo kati ya 220 walioanza.Elimu Mbadala kwa
Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito umefadhiliwai Ubalozi
huo na kuratibiwa na UNESCO.
Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye
kiwango cha juu cha ndoa a utotoni. Kwa wastani, mabinti wawili kati ya
watano huolewa kabla hawajafikisha miaka 18.
Kwa hesabu za mwaka 2010 asilimia 37
ya wanawake wenye umri kati ya miaka 20-24 walikuwa wameolewa au kuwa
na patna anayeishi naye kabla hawajatimiza miaka 18.
Hata hivyo takwimu zinaonesha kupungua kwa asilimia 10 tangu mwaka 2004 ikiwa ni sawa na asilimia 41.
Ingawa ndoa za utotoni ni kawaida
nchini Tanzania mikoa yenye kasi kubwa ni Shinyanga (59%), ikifuatiwa
na Tabora (58%), Mara (55%), Dodoma (51%), Lindi (48%), Mbeya (45%),
Morogoro (42%), Singida (42%), Rukwa (40%), Ruvuma (39%), Mwanza (37%),
Kagera (36%), Mtwara (35%), Manyara (34%), Pwani (33%), Tanga (29%),
Arusha (27%), Kilimanjaro (27%), Kigoma (26%), Dar es Salaam (19%) na
Iringa (8%).
Kama hatua hazitachukuliwa mabinti
1,382,000 ambaow atakuwa wamezaliwa kati ya mwaka 2005 hadi 2010
watakuwa wameshajiingiza katika mahusiano ya kuishi pamoja pamoja na
kuelewa ifikapo mwaka 2030, hasa ikizingatiwa kuwa mwaka 2010 wanawake
764,000 wenye umri kati ya 20 hadi 24 walikuwa wameolewa au kuishi
kinyumba kabla ya kutimiza miaka 18.
Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika
la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta akitoa
salamu za UNESCO kwa niaba ya Mkuu wa ofisi ya UNESCO Tanzania, Zulmira
Rodrigues (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya Mpango wa Elimu
Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili
Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya
Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko (kulia) akiteta jambo na
Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA wakati wa mahafali
hayo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko akitoa nasaha zake wakati wa mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa kikundi cha Ujasiriamali cha Upendo Malunga wakitoa burudani ya shairi kwa mgeni rasmi na meza kuu.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu
ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (wa tatu kulia) na meza kuu
wakikagua kazi mbalimbali za mikono zinazofanywa na wahitimu wa vituo
mbalimbali ndani ya halmashauri ya Msalala wakati wa Mahafali ya Mpango
wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito
unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Second Secretary wa Ubalozi wa
Japan, Noriko TANAKA (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa halmshauri ya
Msalala,Vivian Masangya wakitazama ubora wa vitambaa vya meza
vilivyotengenezwa na wahitimu hao.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa
Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko, Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila, Second
Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA pamoja na Ofisa mipango ya
Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania,
Jennifer Kotta wakikagua kazi mbalimbali zilizofanywa na wahitimu hao
kwenye mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule
kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na
UNESCO.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu
ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (kulia), akiwaunga mkono wakina mama
hao kwa kununua shuka na foronya zilizotengenezwa na mmoja wa wahitimu
hao (aliyebeba mtoto mchanga) wakati wa mahafali ya Mpango wa Elimu
Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili
Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Second Secretary wa Ubalozi wa
Japan, Noriko TANAKA (kushoto) akiwaunga mkono wahitimu hao kwa kununua
Batiki wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana
walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na
kuratibiwa na UNESCO.
Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika
la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta
akinunua batiki kutoka kwa mmoja wa wahitimu Hellena Masalu wa Kikundi
cha Safina Kata ya Segese, mkoani Shinyanga wakati wa Mahafali ya Mpango
wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito
unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya
Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko akiwaunga mkono wahitimu
hao wakati wa sherehe fupi ya Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa
Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa
Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Mmoja wa wakufunzi wa
ujasiriamali halmashauri ya Msalala, Bi. Clemencia Mpuga Ngongo akitoa
maelezo kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum
Mjagila, jinsi kifaa cha "Hydrometer" kinachotumika kupima wingi wa
"Caustic" katika hatua za utengenezaji wa sabuni za kufulia za miche
wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha
shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa
na UNESCO.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu
ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila akikata miche ya vipande vya sabuni
ta kufulia iliyotengenezwa na wahitimu hao.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu
ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila akishuhudia kwa vitendo utengenezaji
wa sabuni za miche uliofanywa mbele yake kudhihirisha wahitimu wameiva
kimafunzo.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu
ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (wa pili kulia) akimkabidhi cheti
Mhitimu wa Lunguya, Shija Vicent wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu
Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili
Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu
ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila akimpongeza Mhitimu wa kituo cha
Lunguya, Fatuma Masaja mara baada ya kumtunuku cheti wakati wa Mahafali
ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za
Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Mhitimu wa kituo cha Lunguya,
Fatuma Masaja ambaye aliyepata ujauzito akiwa shuleni na uliompelekea
kukatisha masomo yake na hatimaye mradi wa elimu mbadala kwa wasichana
walioacha shule kwa sababu za ujauzito kumkomboa kwa kumpa mafunzo
mbalimbali ikiwemo ujasiriamali wa kutengeneza batiki, sabuni, ushonaji
n.k. akifurahia baada ya kutunukiwa cheti chake.
Sehemu ya wakufunzi na wazazi waliohudhuria tukio hilo adhimu.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu
ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila na meza kuu wakiwa katika picha ya
pamoja na wahitimu wa vituo mbalimbali vya halmashauri ya Msalala
vilivyohitimu mafunzo hayo.
Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika
la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta
akimpongeza kwa furaha mmoja wa wakufunzi walioshiriki kufanikisha
mafunzo hayo Bi. Clemencia Mpuga Ngongo wakati wa Mahafali ya Mpango wa
Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito
unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Please share this Blog
Zilizosomwa zaidi.
-
MTOTO RAIA WA NCHINI CHINA MIEZI 7 XIAO WEI (PICHANI)AMEZALIWA AKIWA NA KIUNGO KINGINE KATIKA MAKALIO YAKE KIASI CHA KUIBUA TAHAR...
-
Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba ya Afya cha Eckernforde kilichopo Kange Jijini Tanga kinavyoonekana. Chuo Kikuu cha Tanga Ecke...
-
MTOTO HUYU MIAKA MITATU ALICHUKULIWA NA BABA YAKE KISHA BABA YAKE AKAMZIKA SEBULENI KWAKE AKIWA HAI MWILI ...
-
Mtoto akiswaga ng'ombe Sheluhi mkoani Singida wiki iliyopita kama alivyonaswa na kamera yetu. Watoto kama huyu wakijengewa mazingira ...
-
kumradhi kwa kuzitumia picha hizi Hii ndiyo pikipiki inayodaiwa kuibwa na mwanafunzi huyo. Hiki ni kitambulisho cha mwanafunzi huyo ...
-
Majeruhi wa tukio la mauaji ya wivu wa mapenzi, Francis Shumila, akiwa chumba cha dharura Taasisi ya Mifupa (MOI), Dar es Salaam leo as...
-
Spika wa Bunge Anne Makinda a...
-
Former Prime Minister ... Baroness Margaret Thatcher By JACK LOSH BARONESS Thatcher, Bri...
-
Bibi harusi mtarajiwa Sekela Lusajo Mwaibale akiwa katika pozi la Kinyakyusa wakati wa shehere yake ya kuagwa kabla ya kuolewa na mume wa...
No comments:
Post a Comment