MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, WCF, Masha Mshomba, akizungumza kwenye mkutano na waandishi
wa habari makao makuu ya Mfuko huo barabara ya Bagamoyyo jijini Dar es
Salaam, Agosti 16, 2015. Mfuko huo ulioanzishwa kwa sheria ya bunge
namba 20 kifungu cha 5 ya mwaka 2008, una madhumuni ya kutoa fidia kwa
Wafanyakazi kutokana na ulemavu au vifo viinavyosababishwa na ajali au
magonjwa yatokanayo na kazi sambamba na kukuza mbinu za kuzuia matukio
ya ajali, alisema. (Picha na K-VIS MEDIA)
Mfuko huo ambao umeanza kazi rasmi Julai 1, 2015, lengo kuu ni kutekeleza nia ya Serikali kukabiliana na changamoto za ulipaji wa fidia kwa Wafanyakazi katika mfumo wa utoaji fidia uliokuwepo awali, Mkurugenzi Mkuu Masha alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kiwango kidogo cha malipo ya fidia(kiwango kisichozidi shilingi 180,000) kwa ulemavu wa kudumu na shilingi 83,000 kwa wategemezi endapo kifo kitatokea kwa Mfanyakazi husika. Akinukuu sheria iliyoanzasha Mfuko huo, Masha alisema, kifungu cha pili (2), cha sheria ya fidia kwa wafanyakazi namba 20/2008 Mfuko huu unawahusu Waajiri na Wafanyakazi wote katika sekta ya Umma na Binafsi, Tanzania Bara pekee. "Naomba ieleweke, anayepaswa kuchangia kwa mujibu wa sheria hii ni Mwajiri na sio Mfanyakazi kukatwa mshahara wake." Alifafanua Masha

Waandishi wa Habari kazini
Mwandishi kazini
Masha (katikati), akiwa na Kaimu
Mkurugenzi wa hifadhi za Jamii kutoka Wizara ya Kazi na Ajira, Daudi
Kaali, (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya
Kusimamia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini, SSRA, Ansgar Mushi
Mwandishi kazini
Waandishi wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha
Mkurugenzi Mkuu, akitoa ufafanuzi kufuatia maswali ya waandishi wa habari
No comments:
Post a Comment