Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji, Damian Lubuva akitoa mada jana jijini Dar es salaam kwa
viongozi wa madhehebu mbalimbali waliohudhuria mkutanoni .
Baadhi ya viongozi wa dini
waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na NEC jana jijini Dar es salaam
wakifuatilia mada iliyokuwa zikiendelea.
Wanasekretarieti ya maandalizi ya
mkutano NEC na wadau mbalimbali na baadhi ya waandishi wakifuatilia
mjadala kuhusu wajibu wa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji, Damian Lubuva
akiteta jambo na mmoja wa makamishna wa Tume hiyo Prof Amon Chaligha
jana jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa NEC na wadau mbalimbali.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akitoa mada kuhusu mchakato mzima wa
uchaguzi na hatua zilizofikiwa hadi sasa jana jijini Dar es salaam
wakati wa mkutano wa viongozi wa madhehebu ya dini.
………………………………………………………………………..
Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC
imewaomba viongozi wa dini zote kutumia majukwaa yao kuwaelimisha
wapiga kura bila kuonyesha hisia za kuegemea upande wowote wa mgombea
ili waweze kufanya maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi Mkuuu ujao.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva kwenye Mkutano uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam uliowakutanisha wadau hao wa uchaguzi na
kuwakumbusha wajibu wao katika jamii hususani katika kipindi hiki
ambacho nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.
Alisema kuwa taasisi za kidini
zinaaswa kama walivyo wadau wengine katika kipindi hiki cha uchaguzi
kuhubiri amani na kuendelea kutoa elimu kwa watanzania ili zoezi hili
liishe kwa amani na kuwaacha watanzania wakiwa na umoja na mshikamano
licha ya tofauti za kiimani zilizopo miongoni mwao.
“Tume inawataka, nyinyi
viongozi wa dini, mnapotoa mafundisho ya uchaguzi kwa waumini wenu
kuhakikisha hamuonyeshi hisia za kuwa upande wa chama chochote cha
kisiasa na zaidi kuepuka kushawishi waumini wenu kuegema chama au
mgombea fulani” amesema Jaji Lubuva.
Mmoja wa washiriki wa mkutano
huo , Askofu Philemon Phiri wa kanisa la EAGT-Mikocheni -A ameiasa
Tume hiyo kusimama katika haki, uhuru na kuhakikisha wanatangaza
washindi bila kuonyesha upendeleo ili kuivusha nchi ikiwa salama.
Mshiriki mwingine kutoka Kanisa
la Moravian Mchungaji Alamu Kajuna alisema kuwa amani ndiyo tunu kwa
kila mwanadamu, hatutegemei vurugu wakati huu wa uchaguzi maana amani
inapotoweka wanaoumia ni wananchi wakiwamo waumini wao hivyo wao kama
taasisi zinazoshirikiana na wananchi kwa karibu kuhakikisha wanatoa
elimu kwa wananchi ili tupate viongozi kwa amani
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imekutano na viongozi hao na wadau wengine ikiwa zimebaki siku mbili
kuanza kwa kampeni hapo Jumamosi ijayo kwa ajili ya maandalizi ya
uchaguzi mkuu ujao.
No comments:
Post a Comment