Mratibu
wa Uzazi Salama Kitaifa, Dk. Koheleth Winani akizungumza na waandishi
wa habari za masuala ya haki jinsia na uzazi katika mkutano uliofanyika
leo katika hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR nchini,Siyovelwa Hussein akizungumza na waandishi wa habari wa wa Haki na Afya ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Uzazi Salama Kitaifa, Dk. Koheleth Winani akionyesha katiba ya chama hicho kuashiria uzinduzi wa chama cha TAMENET–SRHR leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Msaidizi wa mradi wa TMEP ,Eugnia Msasanuri akizungumza na wadau wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR.
Wadau wa Mtandao wa
waandishi wa habari wa Haki na Afya ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR
wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI
imesema kuwa imefikia lengo la nne la millenia ya kupunguza vifo vya
watoto chini ya miaka mitano kwa kufikia vifo 54 kwa kila vizazi hai
1,000.
Hayo ameyasema leo Mratibu wa Uzazi Salama Kitaifa,Dk.
Koheleth Winani wakati wa uzinduzi wa mtandao wa waandishi wa habari wa
Haki na Afya ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR nchini,amesema kuazishwa
kwa mtandao kutasaidia kusukuma harakati za kupunguza vifo hivyo.
Amesema
anatambua mchango wa waandishi habari katika mapambano dhidi ya Afya
ya Uzazi na ukatili wa kijinsi pamoja na ukatili dhidi ya watoto.
Dk.
Winani katika kuboresha afya ya uzazi ,kutokomeza ukatili wa wa
kijinsia na ukatili dhidi ya watoto katika kupunguza vifo vya
vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto chini ya miaka mitano.
Aidha
amesema waandishi katika kwa kuazisha wametambua majukumu yao katika
taifa katika harakati za masuala ya afya hususani uzazi.
Kaimu
Mwenyekiti wa Mtandao huo,Siyovelwa Hussein amesema kuwa kuazishwa kw
amtandao huo inatokana na mafunzo mbalimbali pamoja na kujionea hali
halisi katika maeneo ambayo yako nyuma katika masuala ya afya ya uzazi.
Siyovelwa
amesema kuzinduliwa kwake na kuaza kufanya kazi katika kuweza
kujiimarisha kifedha katika kuelimisha wananchi katika masuala ya afya.
No comments:
Post a Comment