Huduma ya kifedha kwa kutumia
njia ya simu ya mkononi ya Tigo ijulikayo kama Tigo Pesa inashirikiana
na kampuni ya Worldremit ya Uingereza inayofanya huduma za kuhamisha
fedha kwa njia ya mtandao ili kuwawezesha watanzania waishio nje ya nchi
kutuma fedha moja kwa moja kuja kwa ndugu, jamaa na marafiki waishio
Tanzania kwa kupitia simu zao za smartphone, tablets na tarakilishi.
Akitangaza wakati wa uzinduzi huo
leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa huduma ya kifedha wa simu za mkononi
za Tigo Ruan Swanepoel alisema, “huduma hii imekuja na tuzo ya iPad kwa
mtu atakayekuwa akipokea kiasi kikubwa cha fedha kwa wiki. Tigo itakuwa
ikitoa jumla ya iPad mbili, moja kila baada ya wiki kuanzia leo,” Ruan
alisema.
Tigo Pesa sasa imekuwa ndiyo njia
ya kawaida kupokea fedha kutoka nchi za nje kuja Tanzania kwa wateja wa
WorldRemit, imekuwa ni zaidi ya kuchukua fedha taslimu,kuongeza muda wa
maongezi na kuhamisha fedha kwenda akaunti ya benki.
Ruan alisema kuwa, “Kushirikiana
kufanya kazi na WorldRemit ni sehemu ya mkakati wa kampuni wa
kuiunganisha kikamilifu huduma ya Tigo Pesa kwa mfumo wa malipo ya
kimataifa. Dira yetu ni kuwafanya wateja wa Tigo Pesa kufurahia kufanya
uhamisho wa fedha usiokuwa na kikomo kitaifa na kimataifa kupitia simu
zao. Huduma ya WorldRemit sio kwamba hutoa tu ongezeko la kasi ya
kuhamisha fedha bali pia hutoa viwango bora ikilinganishwa na huduma
nyingine za kuhamisha fedha.”
Kuna wahamiaji wapatao 250,000
kutoka Tanzania wanaoishi nje ya Afrika. Kwa mujibu wa takwimu za hivi
karibuni za benki ya dunia zinanonyesha kuwa Uingereza,Marekani na
Canada zina idadi kubwa ya watanzania wanaoishi huko.
Benki ya Dunia pia
imeidhihirishiaTanzania kuwa ni muhimu kama soko la kupokea katika
shughuli za ubadilishanaji wa fedha. Kwa mwaka 2014 Tanzania ilipokea
jumla ya dola za kimarekani milioni 64 kutoka kwa Watanzania wanaoishi
ughaibuni. Nchi ambazo zilituma fedha nyingi kuja Tanzania ni pamoja na
Kenya, Uingereza, Uganda, Canada, Marekani, Australia na Afrika Kusini.
Jeff Pietras, Makamu wa Rais wa
maendeleo ya bidhaa za kimataifa katika kampuni ya WorldRemit alisema,
“WorldRemit inabadilisha ulimwengu uliochoshwa na uhamisho wa fedha
kupitia huduma zetu za kimitandao na simu tu. Watu kote duniani wanaweza
kutuma fedha mara moja kupitia akaunti zao za Tigo Pesa kwa kubonyeza
mara chache tu kwenye simu zao za smartphone na kufurahia urahisi na
uwazi wa bei.”
WorldRemit ni huduma inayoongoza
kwenye uhamisho wa fedha mtandaoni kwenda kwenye huduma ya kifedha ya
simu za mkononi, ambayo sasa ni njia inayopendwa kwa ajili ya kupokea
fedha katika nchi nyingi. Uhamishaji wa fedha kwenda huduma ya fedha za
simu za mkononi umekua kwa zaidi ya asilimia 200 barani Afrika mwaka
uliopita, na kuwakilisha zaidi ya asilimia 30 ya uhamisho wote wa
WorldRemit ambayo asili yake ni Ulaya na Marekani.
Ili kuweza kutuma fedha moja kwa
moja kwa wanafamilia au marafiki zao nchini Tanzania kwa kutumia akaunti
za Tigo Pesa, mtu anayeishi nchi za nje anapaswa kutembelea tovuti ya https://www.worldremit.com/en/tanzania/tigo-mobile-wallet – au kupakua kiunga cha WorldRemit kwenye OS au simu za android .
Hii ni huduma ya pili ya
kuhamisha fedha kimataifa kuzinduliwa na Tigo Pesa baada ya uzinduzi wa
mwaka jana wa huduma ya kuhamisha fedha na ubadilishanaji wa sarafu
kwenda Rwanda. Tigo Pesa pia inafanya kazi na huduma za kifedha za benki
ya biashara nchini ili kuwawezesha wateja wa Tigo kuchukua au kuweka
fedha kutoka kwenye simu zao kwenda akaunti zao z
No comments:
Post a Comment