Tunaelekekea kipindi hiki cha
kusherehekea sikukuu ya Eid-El-Fitr na ambapo wananchi wenye imani ya
kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja
na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe,
Jeshi la Polisi nchini linatoa wito kwa wananchi wote kuwa makini na
kusheherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu pasipo vitendo ama
viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Jeshi la Polisi nchini linapenda
kuwaondoa hofu wananchi kuwa, limejipanga vizuri kuhakikisha wananchi
wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu. Ulinzi umeimarishwa
kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na
maeneo mengine yote.
Aidha, tahadhali zichukuliwe kwa
wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara ikiwemo maderera na watembea
kwa miguu, kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na
hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na
kutumia vilevi wawapo kazini.
Jeshi la Polisi linaendelea
kuwasisitiza wananchi kutoa taarifa haraka kwenye vyombo vya dola juu ya
kitu chochote ama mienendo ya watu watakaowatilia shaka mahali popote
kwani taarifa hizo za haraka zitasaidia kuzuia uhalifu kabla haujatokea.
Vilevile wananchi wachukue
tahadhari watokapo kwenye makazi yao, wasiache nyumba wazi ama bila mtu
na endapo italazimika basi ni vema watoe taarifa kwa majirani zao kwa
ajili ya usalama.
TUNAWATAKIA WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA EID –EL-FITR
Imetolewa na: Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment