PICHA ya Kwanza inayoonesha kwa undani
sayari ya Pluto ilivyo imeonyeshwa kwa mara ya kwanza duniani.
Picha hiyo imepigwa na chombo kisicho
na binadamu cha New Horizons ambacho kilisafiri umbali wa kilometa bilion saba
na tano. Chombo hicho jana jumanne kilitua kwenye sayari hiyo.
Katika mkutano na waandishi wa habari
katika chuo Kikuu cha Johns Hopkins kilichopo Maryland Marekani, Mkuu wa
utafiti wa sayari hiyo Alan Stern
hakusita kuonyesha furaha yake.
"Jana ilikuwa ni siku nzuri na ya
kipee kwangu, vipi kwenu.". Mkuu huyo wa utafiti - Alan Stern amesema
chombo hicho cha anga kimekusanya taarifa nyingi kutoka kwenye sayari hiyo.
"Sawa chombo chetu cha New
Horizons kimekwenda sasa zaidi ya mile milioni moja.Zaidi ya kilometa moja na nusu
upande wa pili wa Pluto, hivyo ndivyo tunavyokwenda kwa haraka tumefikia karibu
na sayari hiyo hapo jana asubuhi.
Chombo chetu cha anga kipo katika hali
nzuri, kinafanya mawasiliano na dunia kwa mara nyingine mara kwa mara kwa masaa
kuanzia asubuhi saa 11 na dakika 50. Tayari tumepata data kutoka kwenye vifaa
vya kisayansi vipatavyo vitano, na tutatoa taarifa kuhusu matokeo tuliyopata,
lakini ukweli ni kwamba tunachunguza kwa undani , kuna mengi." Amesema
Alan Stern.
Chombi hicho kiliruka kwa mara ya kwanza
mwaka 2005, ambapo mpaka sasa ni miaka 10.
No comments:
Post a Comment