Na Mwandishi wetu
Mchakato wa uchukuaji fomu za kugombea ubunge katika majimbo mbalimbali
kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakiwamo Ilala, Temeke na kinondoni umeanza rasmi
leo kupitia ofisi za wilaya za chama hicho.
Wanachama waliochukua fomu kwa jimbo la Ukonga ni Jerry Slaa, Jacob Kasema, Hamza Mshindo na
Fredrick Rwegasira, huku waliochukua fomu katika jimbo la Segerea kuwa ni Zahoro
Lyasuka,Apruna Jaka, Bonna Kalu.
Huku Musa Azzan Zungu akichukua kwa jimbo la Ilala na mwenzake wa Wilaya ya Temeke akiwa ni
Mbunge wao Abbas Mtemvu ambaye anagombea jimbo hilo kwa mara nyingine
tena.
No comments:
Post a Comment