Na
Katuma Masamba
Baada
ya CCM kumpitisha John Pombe Magufuli, kugombea Urais, kazi kubwa imebaki kwa
vyama vya upinzani ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kumpata
mwakilishi wao.
Story
ni kwamba Naibu Katibu Mkuu wa Cuf, Bara, Magdalena Sakaya, amevunja ukimya na
kueleza siri ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Lipumba na viongozi wa kuu chama
hicho kutoshiriki kikao cha kumchagua mgombea wa Ukawa.
Sakaya
amewaeleza waandishi wa habari leo katika Ofisi za Chama hicho kuwa Cuf, haina
mpango wa kutaka kujiondoa kutoka (Ukawa) na kwamba maamuzi ya
kumpata mgombea wa urais wa umoja huo yatatolewa baada ya kikao cha Baraza Kuu
la Uongozi la Taifa la Cuf, Julai 25 mwaka huu.
Chama
hicho pia kimekanusha tetesi za kununuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), ili
kiweze kujitoa kutoka Ukawa, hivyo kuudhoofisha umoja huo na kuipa CCM nguvu
katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 25 mwaka huu.
Kabla
ya kutolewa kwa taarifa hizo, juzi, wanachama wa Cuf, walitinga makao makuu ya
chama hicho, Buguruni jijini humo, wakitaka ufafanuzi juu ya habari
zilizochapishwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii kwamba, mgombea wa
urais wa Ukawa, ameshapatikana na idadi ya kura kutolewa, kinyume cha
utaratibu wa umoja huo.
No comments:
Post a Comment