![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJFKJ5rOSbGuETXgH9FAWzMX_eqy0Th-8WUywQ6uWQXbrEbq2Kr7mdyh6nf7KPtqSFpkllJ8Psdcvnyy1j_ubkYU07rEvFvRk6bqWAKqRjJGGsmX78xyDJUH0PYZWVMIVbfzSltCbnpGg/s640/1.jpg)
Mwenyekiti wa shirikisho la elimu ya juu taifa(MNEC) Zainabu Abdalah Issa kushoto Mkamu mwenyekiti Hamid Saleh Mhina.
Na Frank Monyo
Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo ya Elimu ya Juu Tanzania Chama cha Mapinduzi , wamewapongeza wajumbe wa vikao vya maamuzi ndani ya chama kwa kutenda haki na kumteua mgombea safi, muadilifu, mchapa kazi na mzalendo kwenye chama hicho Dk. John Magufuli.
Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo ya Elimu ya Juu Tanzania Chama cha Mapinduzi , wamewapongeza wajumbe wa vikao vya maamuzi ndani ya chama kwa kutenda haki na kumteua mgombea safi, muadilifu, mchapa kazi na mzalendo kwenye chama hicho Dk. John Magufuli.
Hayo yalisemwa
jijini Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa
Shirikisho Taifa Zainabu Issa wakati wa kusoma tamko la Shirikisho hilo la kuwaunga
mkono wajumbe wa mkutano mkuu huo.
Zainabu alisema
wanachukua fursa hiyo kuwapongeza Dk. Magufuli pamoja na mgombea mweza Samia
Suluhu Hassani kwa kuteuliwa kuwa wapeperusha bendera ya CCM 2015 na Dk.Ali
Mohammed Shein kupeperusha bendera ya urais kwenye serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
"Tunawapongeza
wajumbe wote kwa kutenda haki na kumteua mgombea safi, muadilifu mchapakazi,
mzalendo ambaye hakuwa na kundi na ambaye hana kundi hadi sasa tunaamini
atadumisha umoja na mshikamano ndani na nje ya chama chetu,"alisema
Alisema watanzania
wana mategemeo makubwa kwao kwa fursa waliyoipata.
"Kwa uteuzi
huu tunapenda kukipongeza chama chetu chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete
kwa mara ya kwanza katika historia kwa kuwaamini na kuwapa fursa wanawake na
kuwapa nafasi za juu za uongozi wa nchi,"alisema na kuongeza
"Napenda
kuwakumbusha wanachama wenzetu waliojitokeza kuomba ridhaa ya uteuzi wa chama
chetu kuwa mgombea aliyepatikana ni kwa mujibu wa taratibu na kanuni za uteuzi
za chama chetu na si vinginevyo,"
No comments:
Post a Comment