Mkuu
wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akikagua gwaride
maalum la wahitimu wa mafunzo ya JKT yaliyofanyika katika kikosi cha
825 JK Mtibila ambapo vijana 1140 walifuzu na kumaliza mafunzo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akipokea heshima kutoka kwa wahitimu.
Wahitimu wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akizungumza na wahitimu hao wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akiangalia madawati yaliyotengenezwa na vijana hao wa JKT.
**************
Mkuu
wa Wilaya ya Kasulu Col Martin Eliah Mkisi katika hotuba yake,
amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya JKT Oparesheni Magufuli Kundi la
nne Kwa Mujibu wa sheria, kuiamini, kuitekeleza na kuiishi kaulimbiu ya
HAPA KAZI TU.
Amesema
vijana hao waliobahatika kupata mafunzo ya JKT katika kambi ya 825 KJ
Mtabila kuja na mbinu mbadala na mawazo chanya ktk kutatua changamoto
mbalimbali za maisha badala ya kulalamika.
Amewataka
kuwa kielelezo cha nidhamu na uzalendo ktk maisha yao ya vyuoni na
mahali pa kazi hapo baadaye kama walivyofundishwa na Wakufunzi Mahiri wa
JKT.
Aidha,
Col Mkisi amelipongeza JKT kwa kutekeleza wajibu wake adhimu wa kuwalea
na kuwafundisha vijana wa Tanzania, stadi za maisha, uzalenda na
ujasiliamali.Vijana wapatao 1140 walifuzu mafunzo hayo yaliyochukua
miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment