MENEJA wa msanii Diamond Platnumz, Hamis Taletale “Babu Tale”
amefikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akitokea kituo cha
polisi ambako alilala jana baada ya mahakama kutoa amri ya kukamatwa kutokana
na kutotii amri iliyomtaka amlipe Sheikh Hamis Mbonde Sh milioni 250.
Babu Tale ambaye alifika mahakamani hapo mapema kabla ya
kuitwa kwa kesi hiyo iliyoanza saa 10:40
asubuhi, miguuni alikuwa amevalia kandambili huku akisindikizwa na
Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe, Said
Fella pamoja na msanii chipukizi wa Bongo fleva kutoka lebo ya Wasafi Classic
Baby (WCB), Raymond.
Meneja huyo anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja
mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa
kuuza na kusambaza nakala za
mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya Shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki
miliki.
Wakili wa upande wa mdai, Mwesiga...Isome zaidi kesho katika Gazeti la HabariLeo
No comments:
Post a Comment