JUVICUF YAWATAKA VIONGOZI KUWA MAKINI KATIKA KUTOA MAAMUZI - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, July 17, 2016

JUVICUF YAWATAKA VIONGOZI KUWA MAKINI KATIKA KUTOA MAAMUZI

Mkuu wa Habari na Uenezi wa Jumuiya ya Vijana Cuf (JUVICUF), Dahlia Majid akizungumza n awaandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
 
Na Mwandishi Wetu
 
Chama cha wananchi  CUF  kimewataka  viongozi  wa siasa nchini kuwa makini na maamuzi wanayoyafanya katika shughuli za kulijenga taifa yawe  ni maamuzi yenye tija kwa wananchi na sio ya kukurupuka tu.

Akizungumza jijini hapa na waandishi wa habari  mkuu wa habari na uenezi wa jumuiya ya vijana cuf (juvcuf) Dahlia Majid, alisema chama cha wananchi cuf kinasikitishwa sana na tabia ya baadhi ya viongozi kufanya maamuzi ya mlipuko na yasiyo na tija kwa wananchi, kwani tabia hiyo ikiendelea nchi haitakuwa salama na pia kupelekea hatua ambazo si sahihi kwa taifa kama tanzania.

Alisema uteuzi wa viongozi na watendaji katika serikai ni hatua muhimu sana kwa kiongozi yeyote anayeingia madarakani katika kuhakikisha kwamba utawala wake unaenda kuwa na matokeo chanya kwa wananchi na pakitokea udhaifu wa aina yeyote ile madhara yake ni kwa wananchi  kwani viongozi hao watakosa tija kwenye maendeleo ya taifa.

‘’Jumuiya ya vijana imepokea kwa mshangao mkubwa uteuzi uliofanywa na Rais John Magufuli kwa kuwateua makada wa ccm  katika nafasi ambazo si za kisiasa na badala yake ni nafasi za kiutumishi wa umma ambapo zinapaswa kushikwa na wataalamu badala ya wanasiasa ,juvicuf haikusudii kuhoji uhalali wa raisi kuteua wanasiasa hao na kuwaingiza katika utumishi wa umma,juvicuf imepata mshtuko unaosababishwa na dhana ya neno‘;utumishi wa umma’’’’alisema MAJID’’

Majid alisistiza kuwa uzembe huo umeendelea hata katika ngazi za chini  huku akitolea mfano mwezi machi 2016 waziri wa nchi ofisi ya wazir mkuu,sera,bunge,kazi,vijana ,ajira na wenye ulemavu,Jenister Mhagama alitengua uteuzi wa kaimu mkurugenzi mkuu wa shirika la hifadhi ya jamii NSSF dakta Catarina Wagwe, masaa machache baada ya kuteuliwa siku hiyo hiyo kwa madai ya kutokamilika kwa baadhi ya taratibu.

Mfano wakurugenzi pamoja na kuwa ndio maafisa ajira katika wilaya zao,lakini pia wao ndio huwa wanatumiwa na tume ya taifa ya uchaguzi kuwa wasimammizi katika wilaya zao .
 
Aliongeza kuwa juvicuf inajipanga kuandaa kongamano la kitaifa  ambapo itawaomba maafisa wa tume waje kutolea ufafanuzi suala hilo  na kuwaomba watanzania wote kuwaunga mkono katika hoja hiyo ambayo  inabeba hatima na wigo mpana wa demokrasia ya nchi yetu.

Akifafanua kuhusu agizo la Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, juu ya agizo la kukamata wakazi wa Dar es salaam wasiokuwa na kazi maalumu ya kufanya, alisema hayo ni miongoni mwa maagizo ya kipuuzi ambayo yanatolewa na viongozi nchini  kwani wakati vijana wanahangaika mitaani kutafuta kazi, ni ajabu sana kwa kuwa serikali imefanya maisha kuwa magumu na ajira kuwa ngumu kupatikana sasa inakuwaje serikali kuibuka na sera ya kukamata watu wasio na ajira alihoji ‘’

‘’Haiwezekani viongozi wa awamu ya tano wanakurupuka tu na matamko  yasiyokuwa na tija kila siku tena mengine yanabaka mammlaka hata ya Mahakama lakini wanajifanya wao ndio polisi,wao ndio mahakama na wao ndio magereza alisema Majid’’

Alisema jumuiya hiyo inawasihi vijana waendelee na shughuli zao za kupambana na maisha bila kujali matamko yanayotolewa na viongozi waliolewa madaraka na kujifanya miungu kana kwamba wao ndio wanashikilia maisha ya kila mtu.

‘’Hii nchi ni ya wananchi tunaitaka serikali ya awamu ya tano iache kuharibu nchi na kuwavuruga wananchi na juvicuf tunakitaka chama cha cuf kuwaagiza viongozi wake waache mara moja kutekeleza maagizo yasiyo na tija kutoka kwa viongozi waliolewa madaraka alisema’’

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here