Diwani wa Kata ya Kilungule iliyopo Mbagala
wilayani Temeke, Said Fella,akichimba msingi wa ukuta wakati wa ufunguzi wa
ujenzi wa uzio wa zahanati ya kata ya kilungule,jijini Dar es Salaam, jana. Watatu
kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule, Barnabas Kayuni.
Na Mwandishi Wetu
WANANCHI
wa Kata ya Kilungule iliyopo Mbagala wameshauriwa kujitokeza na kuwa
mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya kijamii ili kuondokana na kero
ambazo zinawezekana kuzitatua wakishirikiana na viongozi wao na kuacha
tabia ya kusubiria na kutegemea msaada kutoka serikalini.
Hayo
yamesemwa na Diwani wa kata hiyo,Said Fella,wakati wa ufunguzi wa
kujenga uzio wa eneo la itakapojengwa zahanati ya Kilungule iliyopo
katika Mtaa wa Kilungule,Mbagala,jijini hapa jana ambapo alisema ombi la
kujengwa zahanati katika kata ya Kilungule imekuja kufuatia usumbufu na
umbali wa kilometa kumi ambazo wananchi wanakumbana nazo wakati
wakihitaji huduma ya afya ambayo huelekea katika hospitali ya Zakhiem
iliyopo Mbagala Rangi tatu na kusema amechangia matofali 1000 kwa ajili
ya uzio huo ambapo halmashauri ya manispaa ya Temeke imekubali kuweka
jengo lake katika eneo hilo.
Ameongeza
kwa kusema kuwa wameamua kutengeneza uzio wa zahanati hiyo kwa nguvu za
wananchi wa kata hiyo kabla ya ujenzi wake ambapo katika jengo hilo
kutakuwa na sehemu ya kujifungulia kwa akinamama,matibabu madogo madogo
na sehemu ya kuhifadhia maiti (Mochwari) ambayo itakuwa msaada mkubwa
kwa wakazi wa kata ya kilungule na kata jirani na kupunguza matumizi ya
fedha kuhudumiwa na kuhifadhi miili ya watu katika hospitali ya Zakhiem
ambako kuna umbali mrefu wa kilometa 10.
“Kupatikana
kwa Zahanati katika kata yetu itatupunguzia matumizi ya fedha kwenda
kuhudumiwa katika hospitali ya Zakhiem pale Mbagala Rangi Tatu lakini
pia itawasaidia akinamama kuondoa hofu ya kupoteza maisha kutokana na
uzazi wakati wa kujifungua,matibabu kwa wananchi wote maana sisi sote ni
wagonjwa watarajiwa pamoja na sehemu ya kuhifadhia miili yetu endapo
hata mimi Said Fella mungu akinichukua nitahifadhiwa hapa hivyo nawaomba
wanakilungule wote tujitoe kuhakikisha zahanati hii inapatikana”
Alisema Fella
Aidha
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilungule,Barnabas Kayuni,alisema kuwa wao kama
serikali watatumia akili zao kuwashawishi wananchi kujumuika na
kuchangia maendeleo katika mtaa wao ili kutatua kero za kijamii ikiwemo
hilo la ujenzi wa uzio wa zahanati ya Kilingule.
Pia
Mwenyekiti wa Nzasa A,Mzee Shefa,alisema katika mitaa mitano ya kata ya
kilungule walikubaliana wachangie ili kumsapoti diwani wao kwa kuwa na
kutoa mfano unapoenda kuomba mboga kwa mwenzako lazima uwe na mboga yako
iliyochacha.
Akizungumza
kwa niaba ya akinamama wa kata hiyo,Uyaone Msonogole,alisema wanawake
wengi wanapata tabu wakati wa kujifungua wengine wanajifungulia njiani
wakipelekwa hospitali ya Zakhiem iliyopo Mbagala ambapo ni kilometa 10
kutokana kutokuwepo kwa zahanati katika mtaa,pia umbali huo umekuwa
ukiwapotezea muda ambao wangeutumia katika kujiongezea kipato na
kujiinua kiuchumi.
Hadi
kumalizika kwa ujenzi wa uzio wa zahanati hiyo yanahitajika matofali
6700 yenye thamani ya Sh.Milioni 7 ukijumlisha simenti na vifaa vingine
jumla yake ni milioni 70,wadau waliochangia ujenzi huo ni Tawi la
Kilungule CCM wamechangia matofali 200,marafiki wa kata hiyo
Sh.707,000,Kikundi cha Akinamama “Amani Federation” matofali 100,Mzee
Muhenga matofali 200 wananchi wote wameombwa kujitolea kuchangia ujenzi
wa uzio huo.
No comments:
Post a Comment