Mpiga picha wa Gazeti la Tanzania Daima, aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Mwangosi Joseph Senga enzi za uhai wake.
NI simanzi na majonzi, siku moja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Iringa kumhukumu kifungo cha miaka 15 askari aliyemuua mwandishi Daudi Mwangosi, tasnia ya habari imepata pigo kwa kuondokewa na mpiga picha wa Gazeti la Tanzania Daima, aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Mwangosi, SHUJAA JOSEPH SENGA, aliyefariki dunia jana usiku.
Senga amefia nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Mojawapo ya picha za tukio la mauaji ya Mwangosi alizopiga Joseph Senga.
Daudi Mwangosi enzi za uhai wake.
Senga, Senga, kamsalimie Daudi Mwangosi, mwabie aliyemuua naye kahukumiwa jela miaka 15, kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado magumu.
Nenda Senga, picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi.
No comments:
Post a Comment