Mgeni
rasmi Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Juma Reli akitoa
nasha wakati akifungua mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta za
maendeleo nchini wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar ambao umefanyika katika Hoteli ya
Zanzibar Ocean View.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho katika Mkutano wa wadau wa sekta za
maendeleo nchini wanaojadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar ambao umeandaliwa na ESRF kwa
kushirikiana na Tume ya Mipango Zanzibar chini ya ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
SERIKALI
ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuhakikisha mipango yote ya
kimaendeleo inayochagizwa na malengo endelevu ya kimataifa inatekelezwa
kwa vitendo ili wananchi waweze kunufaika.
Aidha, imesema
katika malengo ya milennia ya 2015 serikali ilifanikiwa katika baadhi
ya sekta zikiwemo sekta za elimu, afya na miundo mbinu hatua
zinazotakiwa kuendelea kupewa kipaumbele na wadau wa maendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Juma
Reli katika Mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wanaojadili
utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani humo.
Mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
Alisema
licha ya kuwepo na changamoto mbali mbali za kiutendaji katika
utekelezaji wa mipango hiyo ikiwemo suala la wananchi kutokuwa na uelewa
mzuri wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya dunia bado mamlaka husika
zinaendelea kutoa elimu hiyo.
Reli
alieleza kwamba malengo na mipango mbalimbali ya maendeleo ni
kuwasaidia wananchi wa Zanzibar waweze kuondokana na tatizo sugu la
umaskini, magonjwa na changamoto za kiusalama.
“Katika
MDGs tumeweza kufanikiwa kwa baadhi ya malengo ikiwemo suala la elimu na
afya lakini kuna mengine bado hatukuweza kufanikiwa kuyafikia na kwa
sasa tunaendelea na malengo mapya ya SDG’s ambayo tunatakiwa kuyafanyia
kazi ili yaende sambamba na mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.” alisema Reli.
Aidha
alisema bado wanajadiliana ni kwa namna gani mipango ya kimataifa
tutaiingiza katika sera na mipango yetu ya kimaendeleo ili wananchi
waweze kunufaika na fursa hizo za kimaendeleo na kiuchumi kwa ufanisi
zaidi.
Alisema
utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s ambayo ni 17
yanatakiwa kupewa kipaumbele kwani yanagusa nyanja mbalimbali za kijamii
yakiwemo maisha halisi ya wananchi wanaostahiki kunufaika na fursa na mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Mwakilishi
wa Umoja wa Mataifa (UN) Ofisi ya Zanzibar, Anna Senga akizungumza kwa
niaba ya Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro
Rodriguez katika mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini kujadili
utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar.
Kwa
Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafti, Uchumi na
Kijamii nchini ( ESRF), Dkt.Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho
alisema, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika SDG’s ni vyema sera
na mipango endelevu ya nchi husika iweke vipaumbele vya kukuza uchumi
kuanzia ngazi za chini
Kida
alieleza kwamba katika utekelezaji wa SDG’s lazima kuwepo na mpango
endelevu wa ufuatiliaji kuanzia ngazi za chini hadi taifa kwa lengo la
kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa kwa mujibu wa matakwa ya malengo
ya kimataifa.
Naye
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Ofisi ya Zanzibar, Anna Senga
alisema endapo malengo ya dunia yataweza kutekelezwa ipasavyo Zanzibar
itaweza kupunguza changamoto mbali mbali zinazokabili sekta za kijamii
na kiuchumi.
Alisema
UN itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar katika utekelezaji wa SDG’s kama ilivyokuwa katika utekelezaji
wa malengo ya dunia MDG’s yaliyopita ili serikali iweze kufikia ngazi
za chini kwa kuinua kipato cha wananchi kiendane na ukuaji wa uchumi wa
nchi.
Senga
aliishauri serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuendelea kuwashirikisha
wananchi wa ngazi za chini katika kupanga na kutekeleza maendeleo yao
katika maeneo husika ya wananchi.
“Changamoto
zinazojitokeza katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya kimataifa
ili yaendane na mipango ya maendeleo ya serikali ni upungufu wa
ushirikishwaji wa wananchi ama jamii husika na wengine hawafikiwi kabisa
katika maeneo yao jambo linalotakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka katika
kutekeleza kwa vitendo Malengo ya Maendeleo Endelevu ya SDG’s”,
alifafanua Senga.
Naye
Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo (UNDP) Tanzania, Rogers Dhliwayo alisema Malengo ya Maendeleo
Endelevu SDG’s yanatakiwa yawekewe vipaumbele mbalimbali vya takwimu na
tafti za kiuchumi katika maeneo tofauti ya jamii ili malengo endelevu
yaweze kuwafikia walengwa.
Kwa
upade wa washiriki wa mkutano huo kwa nyakati tofauti walisema kwamba
mipango mbalimbali ya kimaendeleo inayopangwa na serikali inatakiwa
kuwekewa vipaumbele kwa wananchi badala ya utekelezaji na tathimini
kubakia ngazi za serikali kuu pekee.
Walisema
kwamba katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s ni
lazima kutengeneza mpango mkakati wa mawasiliano wa masuala ya
utamaduni, mila na desturi za jamii husika ambapo mipango hiyo inatakiwa
kutekelezwa ili iwe rahisi wananchi kufahamu vizuri umuhimu wa mipango
hiyo.
Washiriki
hao walisema katika utekelezaji wa mipango hiyo ni lazima kuwepo na
mikakati ya makusudi ya kuhakikisha changamoto ya umasikini uliokithiri
unapungua kulingana na mikakati mbalimbali inayowekwa na vipaumbele vya
kimataifa ili viweze kutekelezwa kwa vitendo na nchi husika.
Aidha
wameshauri kwamba katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu
SDG’s ni lazima kuzingatia suala la serikali za mitaa, kutumia lugha
nyepesi katika mawasiliano, kufanya marejeo katika maandiko ya baadhi ya
waasisi wa kitaifa akiwemo Mwalimu Nyerere na kufanya utafiti juu ya
matumizi sahihi ya Rasilimali.
Pichani
juu na chini ni wadau wa sekta za maendeleo visiwani Zanzibar
walioshiriki katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya
Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani humo ambao umefanyika katika Hoteli
ya Zanzibar Ocean View.
Sambamba
na hayo wamesema katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDG’s) ni lazima kuweka kipaumbele kwa makundi maalum ya watu wenye
mahitaji maalum wakiwemo Watu wenye Ulemavu.
Warsha
hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF)
ambapo imewakutanisha wadau mbalimbali kujadili utekelezaji wa Malengo
ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar na kufadhiliwa na
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mshauri
wa Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP)
Tanzania, Rogers Dhliwayo akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa
sekta za maendeleo nchini wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya
Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar.
Kutoka
kushoto ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN) Ofisi ya Zanzibar, Anna
Senga, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Balozi Celestine Mushy, mgeni rasmi Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango
Zanzibar, Juma Reli, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi
na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa
Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,
Anna Mwasha wakiwa meza kuu.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na
Watoto ya visiwani Zanzibar, Mauwa Makame Rajab akitoa maoni katika
mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wa kujadili utekelezaji wa
Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar uliofanyika
katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine
Mushy (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Juma
Reli wakisikiliza maoni ya wadau yaliyokuwa yakiwasishwa kwenye mkutano
kuelekea utekelezaji wa SDGs.
Bw.
Sefu Mwinyi kutoka Tume ya Mipango Zanzibar akiwasilisha maoni yake
katika mkutano huo uliowakutanisha wadau wa sekta za maendeleo visiwani
Zanzibar.
Katibu
Mkuu Wizara ya ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani Zanzibar, Khadija
Juma (kushoto) akichangia hoja katika mkutano huo. Kulia ni Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora visiwani
Zanzibar, Asha Abdallah Ali.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment