TUNDU LISSU ALALA RUMANDE KWA KUKOSA DHAMANA - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, June 29, 2016

TUNDU LISSU ALALA RUMANDE KWA KUKOSA DHAMANA

 
 
 
 
 
 
 
Na Mwandishi Wetu
 
MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amejikuta akilalala rumande baada ya kukosa dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central)  jijini Dar es Salaam.
 
Hatua ya Lissu kulala rumande imekuja siku moja baada ya kuachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu ambako anakabiliwa na mashitaka ya kuchapisha taarifa za uchochezi katika gazeti la Mawio.
 
Lissu ambaye alifika katika kituo hicho majira ya saa 7:30 mchana alihojiwa kwa saa tatu kutokana na kauli yake aliyotoa baada ya kuachiwa kwa dhamana katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na maneno aliyoyaandika kupitia mitandao ya kijamii.
 
Mwanasheria wa Tundu Lissu, John Mallya alisema Lissu atalazimika kulala rumande baada ya kunyimwa dhamana na kama kesho atafikishwa Mahakamani watahakikisha wanakuwepo ili kumsimamia kupata haki zake za kisheria.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here