Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la
Umeme Tanzania (Tanesco) limetenga zaidi
ya Sh bilioni 517 ya mapato yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017 katika
utekelezaji wa miradi yake mikubwa ikiwemo asilimia tatu wakipeleka kwa wakala
wa Umeme Vijijini (REA).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Eng. Felchesmi Mramba, fedha hizo zitalifanya shirika hilo kuwa na zaidi ya Sh bilioni 969 walizotenga kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya shirika hilo ambapo Sh.bil.449
zitatolewa na Serikali kuu pamoja na wahisani.
Mramba aliitaja baadhi ya miradi itakayotekelezwa kuwa ni pamoja na pamoja na utanuzi wa vituo vya kupoozea umeme, ununuzi wa Transfoma kubwa na mpya, utengenezaji wa njia
za usambazaji umeme ambapo kwa fedha za
sasa za mapato ya ndani zinajenga njia
za umeme kutoka Mtwara na kuunganisha mkoa Lindi.
Alisema kuwa
asilimia tatu ya makusanyo ya shirika hilo zinapelekwa REA kwa ajili ya kusaidia miradi inayotekelezwa na
wakala hao ambapo katika mwaka uliopita
TANESCO imechangia kiasi cha Sh. bil 50 katika miradi.
Katika
hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.James Mdoe alisema wanapozungumzia Tanzania kuwa nchi ya viwanda
ni pamoja na upatikanaji wa umeme wa kutosha.
No comments:
Post a Comment